*************************
Adeladius Makwega
Zanzibar
Makabila ya kiafrika yana mambo mengi ambayo yanaweza kuwashangza watu katika maisha yao. Kabila la Wayao lipo tofauti sana katika mahusiano kwa mfano baina ya Bibi na mjukuu juukuu na babu na mjukuu wake. Kwa hakika hakuna mahusiano ya utani baina yao. Bibi huwa sawa na mama na babu huwa sawa na baba.
Swali la kujiliza kuikoni Wayao hakuna mahusino ya utani baina ya mjukuu babu na bibi zake? Kulijibu swali hilo kuwa mara baada ya mtoto kuzaliwa. Baba na mama wa mtoto humlea mtoto huyo kwa umri kata ya mwaka mmoja hadi saba.
Kuanzia umri huo na kuendelea mtoto huyo anapelekwa kwa babu na bibi yake kulelewa. Malezi hayo huwa kama yale ya baba na mama yake na siyo malezi ya kudekezwa kama yalivyo kwa makabila mengine kwa babu na bibi wakilea mjukuu.
Kwa desturi ya makabila mengine mjukuu anayelelewa na babu huwa anapata upendeleo mkubwa. Mjukuu hufaamika kama (Wisukulu) na Babu huitwa Ambuje. Hapo wanaweza kuitana kama Chemwali (dada) achimwene (kaka).
Mjukuu wa Kiyao unaweza kumsikia kuwa:
“Ngenda kwa achimwene.” Naenda kwa kaka yangu. Kiukweli anakwenda kwa babu yake.
Katika kabila la hili inaaminika kuwa mtu ambaye si jamaa yako kwa damu hawezi kukuloga, ndiyo kusema kwa mchawi ni yule unayezaliwa na weye. Jambo hilo linafanya Wayao wengi wamekuwa wavivu sana kufanyiana ubaya wenyewe kwa wenyewe na hata imekuwa adimu kumtakia Myao mwenzake mabaya hadharani kwa kuogopa hilo.
Jambo hilo limefanya hata ndugu hawa kukwepa kufanyiana mabaya na hata kutamkiana mabaya. Hilo linaweza kutokea kwa sasa labda mtu huyo awe amekulia pahala pengine na amekwenda huko ukubwani. Hata kama amezaliwa pahala pengine wazazi wake wanapompeleka akiwa na umri wa miaka saba basi mtoto hujifunza mila zote za wazee na kubwa kuhakiisha kuwa nduguyo ndiye mchawi. Lazima kumpa heshima yake.
Kwa kanuni hiyo ya Kiyaoni kuwa huwa hawamuogopi mgeni, wao wanaogopana na wenyewe kwa wenyewe.
Kijana ambaye hajaoa huitwa Buruda hii ikitokana na neno ya Kijerumani bruder, binti ambaye hayaolewa huitwa sista ikitokana naneno ya kiingereza sister.
Athari ya matumizi ya maneno haya huwa ni moja tu kwa kuwa Kanisa Katoliki liliweka mizizi huko kwa hiyo inatokana na wale watawa wa kikataoliki kutumiwa majina hayo kwa muda mrefu na kuwa sehemu ya maisha ya Wayao.