MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza katika kikao na watumishi wa halmshauri ya Kondoa Mji mkoani Dodoma ambapo hajaridhishwa na ujenzi wa Madarasa.
Baadhi ya watumishi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa kikao na watumishi wa halmshauri ya Kondoa Mji mkoani Dodoma ambapo hajaridhishwa na ujenzi wa Madarasa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Chemchem,Juma Yusufu Stambuli,,akizungumza katika kikao cha watumishi wa halmshauri ya Kondoa Mji mkoani Dodoma wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bicha,Iddy Ramadhani Abdallah,akizungumza katika kikao cha watumishi wa halmshauri ya Kondoa Mji mkoani Dodoma wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.
………………………………………………………
Na.Erick Mungele,Kondoa
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amesema hajaridhishwa na ujezi wa madarasa yaliyojengwa na halmshauri ya Kondoa Mji mkoani Dodoma, kutokana na kujengwa chini ya kiwango,
Mtaka,aliyabainisha hayo juzi wakatiki wa kikao cha kazi pamoja na watumishi wa halmashayi hiyo.
Mtaka amesema kuwa madarasa hayo ambayo yalikuwa yajengwe ndani ya siku 90 badala yake yamejengwa na siku za nyongeza na kwa kiwango chini.
Kutokana na hali hiyo aliwataka viongozi wa halmashuri hiyo ya Kondoa Mji kuwa na ushirikano na kuacha migogoro inayosababisha kurudisha nyuma maendeleo.
“Nawapongeza kwa kumaliza ujenzi wa madarasa kwa hela mliyopewa na kumaliza kujenga madarasa hayo 24 lakini sijaridhishwa na ujezi wa madara hayo licha ya kutomaliza kwa wakati na kupewa siku za nyongeza mmejenga chini ya kiwango, “amesema Mkata
Amesema kuwa badala ya kuendelea kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija watumishi wa halamashauri hiyo watengeneze hoja zitakazo leta maendeleo katika halmashauri yao kama vile kuboresha sekta ya elimu na uchumi na kuleta ushindani.
“Kondoa inaoneka mnapenda sana migogoro kitu kinachofanya kurudisha nyuma maendeleo ya halmashuri hii ingekuwa ni vyema mnatumia muda wenu kutoa hoja za kimaendelea katika elimu na mapato namna gani ya kushindana na halmashuri nyingine na ikizingatiwa nyie manakata 8 tu.
Viongozi wa halmashauru hiyo waliomba kuongezewe gari la taka kutokana na mahitaji kuwa mengi na gari ni moja huku idadi ya watu ikiendlea kuongezeka kila siku.