Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza wakati wa kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani) kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), Jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), na viongozi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifuatilia kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani), wakijadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 (sh. trl. 7) zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) akizungumza wakati wa kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani) kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (Mb), akizungumza wakati wa kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani) kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na viongozi wa wizara baada ya kukamilika kwa kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah,(hayumo pichani) kilichojadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, jijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ukifuatilia kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani) wakijadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Katikati), akijadiliana jambo na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) (Kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (Mb), baada ya kuhitimisha kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akijadili jambo na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) (Kushoto), wakati wa kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, (hayumo pichani), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
**********************
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya mazungunzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada unaokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 3 sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 7 zitakazotolewa na Benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akizungumza katika mkutano huo uliowashirikisha pia Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imeazimia kuuelekeza mkopo huo kwenye miradi 32 iliyoko Bara na Visiwani katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo cha umwagiliaji, maendeleo ya mifugo, upanuzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu-Zanzibar (SUZA) na uwezeshaji wa Serikali za Mitaa.
Aidha, Dkt. Nchemba alibainisha kuwa pamoja na uwekezaji wa fedha hizo katika miradi ya kimkakati itakayosaidia kukuza ajira na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi, mkopo na misaada hiyo itasaidia kuendeleza sekta binafsi kwa njia ya ukuzaji biashara ya uagizaji kwa sekta binafsi na usafirishaji wa bidhaa kwa taasisi za kifedha nchini.
Aliwaagiza wataalam mbalimbali Serikali ikiwemo Wizara ya Kilimo kuainisha sehemu ya eneo la Hekta milioni 29 linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa na maandiko ya kitaalam yanayohusu maeneo hayo ili yaweze kupatiwa fedha.
Naye Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alisema kuwa fedha kutoka BADEA zitasaidia kuendeleza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwenye miradi 19 ili kuongeza tija katika eneo la umwagiliaji linalokadiriwa kufikia hekta milioni 1.2 kati ya Hekta milioni 29 zilizopo hivi sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dr. Sidi Ould Tah, alisema Benki yake imejipanga kutoa kiasi hicho cha fedha cha dola za Marekani bilioni 3 na kwamba atatuma timu ya wataalam kutoka Benki hiyo kuja nchini itakayoungana na timu ya wataalam wa ndani ili kujadili kwa kina zaidi namna ya kutekeleza mpango huo.