Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Ndalahwa Gunze akizungumza wakati wa Kutoa hukumu kwa Kituo cha Big Star Radio kwa kukiuka maudhui mtandaoni ,Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Ndalahwa akimkabidhi nakala ya hukumu kwa Mwakilishi wa Big Star Radio,jijini Dar es Salaam.
*******************
TCRA yaipiga Big Star Radio faini ya sh.Milioni Moja.
KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeipiga faini ya sh milioni moja Radio Big Star kwa kutangaza Maudhui yenye uchonganishi, upotoshaj, uchochezi dhidi ya mihimili ya serikali na bunge katika sakata la Spika Ndugai hivi karibuni.
Big Star Radio iliunganisha Stori wa Waziri Mkuu na Storo Katibu Mwenezi wa Njombe wa CCM kwa kile kilichodaiwa habari hiyo haikufuata mezania na kuwa habari hiyo haikuwa sawa kuunganisha na Waziri Mkuu mkoani Lindi.
Aidha imeamuru kampuni hiyo kuomba radhi kwa umma wa watanzania kwa kutangaza maudhui yaliyokiuka sheria na kanuni kupitia channel yao ya maudhui mtandao iliyotumika kutenda kosa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari 13 mwaka
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Ndalahwa Habibi Gunze amesema hayo alipokuwa akitoa uamuzi wa Kamati ya Maudhui kuhusu mashtaka ya ukiukaji wa kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Maudhui ya Mtandaoni 2020.
Gunze amesema Januari mosi mwaka huu, kituo hicho kilikiuka sheria, kanuni na maadili ya utangazaji wa habari kupitia channel yake ya YouTube kwa kutangaza Maudhui yenye lengo la kuchonganisha mihimili ya serikali na bunge.
” Muandaaji wa kipindi alirusha Maudhui yenye uchonganishi, upotoshaji, uchochezi, uongo na tuhuma zisizo na uthibitisho na ambazo hazijatolewa ufafanuzi kwa kuonyesha taarifa ya Waziri Mkuu, Majaliwa akiwa anaongea na waumini wa dini ya kiislamu mkoani Lindi,
Mwenyekiti alinukuu taarifa hiyo “Akiwaambia madaraka yanatoka kwa Mungu na mtu hutakiwi kulazimisha kupata madaraka. Baada ya kauli hiyo, muandaaji wa kipindi aliweka picha jongevu ya Erasto Ngole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, mkoani Njombe akitoa maneno ya kumkashifu na kumshutumu Soika wa Bunge Job Ndugai,” alisema.
Alisema kwa kitendo cha kutangazia umma taarifa za upotoshaji, kashfa na zisizo na uthibitisho na ambazo hazijatolewa ufafanuzi , kampuni hiyo inatuhumiwa kukiuka kanuni .
Alisema pia Kamati inashauri kampuni hiyo kuhakikisha inakuwa na usimamizi makini wa Maudhui yao kabla na baada ya kuyatangaza ili kuepuka makosa.