………………………………………….
Na Lucas Raphael Tabora
Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo ya dhahabu yaliopo katika kijiji cha Nsungwa kata ya Silambo Tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua mkoni Tabora
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana kamamda wa polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao alisema tukio hilo,lilitokea januari 8 mwaka huu majira ya saa 8 alasiri.
Alimtaja mtu aliyefariki kuwa ni Paul Kagatwa (30) mkazi kijiji cha Igwisi wilayani humo alikuwa akichimba Dhahabu kwenye shimo mgodini hapo ndipo alipoangukiwa na kifusi na kuvunjika mguu wa kulia na kupelekea kifo wakati anapelekwa kwenye kituo cha afya Ulyankulu kwa ajili ya matibabu.
Kamanda huyo wa Polisi alisema kwamba mwili ya marehemu ulipofanyiwa uchunguzi na Daktari na kubaini chanzo cha kifo ni kuvujia damu kwa ndani .
Kamanda Abwao alisema mwili wa marehemu umekabidhiwa Ndugu zake kwa ajili ya urartibu za mazishi .
Aidha alitoa wito kwa wachimbaji madini wote kuchukua tahadhari za kiusalama katika mashimo yao, hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea mkoani Hapa
Hata hivyo kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Tabora alisema ipo haja kwa sasa wenye machimbo ya au wamiliki wa migodi hiyo kuchukua taadhari kubwa ili kuepusha vifo vinavyoweza kusababisha madhara kwa wachimbaji wadogo .