Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisalimiana na Watumishi wa Wizara yake mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akisalimiana na mmoja wa watumishi mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi ya Wizara hiyo leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu), Prof Caroline Nombo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na Watumishi wa Wizara yake mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa Watumishi wa Wizara yake mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga,akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi ya wizara hiyo leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka wakati akizungumza na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi ya wizara hiyo leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu), Prof Caroline Nombo,akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja Katibu Mkuu wake kuwasili rasmi katika ofisi ya Wizara hiyo leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
……………………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amewataka watendaji wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ujasiri bila woga ili kukidhi matarajio ya watanzania kwenye ubora wa elimu.
Prof.Mkenda ameyasema hayo leo Januari 10,2022 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo Mtumba mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.
“Kwa wafanyakazi wote naomba tu tufanye kazi kwa ujasiri, bila woga, utii, uaminifu na uadilifu, tusifanye kazi kwa nidhamu ya woga, ukaogopa sana kufanya maamuzi ambayo ni sahihi,”amesema.
Aidha, amesema wao viongozi wana wajibu wa kuwajibika kwa kuwa wizara ikiyumba anayelaumiwa ni mmoja.
“Tusaidiane tusiyumbe , najua kabisa tunahitajika sana kujibu kiu ya watanzania najua kazi imeanza, najua Waziri Prof.Joyce Ndalichako na aliyekuwa Katibu Mkuu Dk.Akwilapo na timu hapa mmeshaanza mchakato hatuanzi kwenye sifuri tunakuja kupanda mabega ya majabali waliosimama, tuna faida ya watangulizi wetu kwa hiyo tumalizie hiyo kazi hasa ya ubora wa elimu,”amesema.
Prof.Mkenda amesema Ilani ya uchaguzi ya CCM imezungumzia masuala ya maendeleo ya teknolojia hivyo wana majukumu makubwa na kuhimiza kufanya kazi kwa ushirikiano.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof.Eliamani Sedoyeka, amesema matumizi ya teknolojia katika elimu ni kati ya vitu ambavyo anaviishi.
“Nategemea ushirikiano kutoka kwenu tushirikiane tuchape kazi na kazi iendelee,”amesema.













