Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuff Masauni akiwasili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo, tarehe 10 January 2022, Mtumba, mkoani Dodoma na kupokelewa na baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne A. Sagini akipokelewa na baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, leo, tarehe 10 January 2022 , Mtumba mkoani Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhani Kailima, leo tarehe 10 January 2022 Mtumba, mkoani Dodoma wakisubiri kuwapokea Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Y. Masauni akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo, tarehe 10 Januari 2022, Mtumba mkoani Dodoma. Ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuendelea kufanya kazi vizuri.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne A. Sagini akizungumza na Menejiment na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo, tarehe 10 January 2022 Mtumba, mkoani Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
*************************
Na Mwandishi wetu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuph Masauni, ameipongeza Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa kazi nzuri ambazo wameendelea kuzitekeleza katika Wizara hii.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo leo wakati akipokelewa rasmi katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Doodoma, baada tu ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani.
“Ni Imani yangu tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa letu, mara zote ushirikiano ndio unaoweza kufanikisha kuondoa changamoto mbalimbali zinazotukabili’ amesisitiza Mhandisi Masauni.
Waziri Masauni amewataka watendaji na watumishi wa Wizara hiyo, kutosita kutoa ushauri katika jambo lolote ambalo likitekelezwa litaleta ufanisi na mafanikio ya kiutendaji katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Amesisitiza kuwa kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano ndio msingi wa mafanikio katika kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, amesisitiza Watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kutatua changamoto zozote zile zinazoikabili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.