********************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imefanikiwa kufuzu FAINALI katika michuano ya Mapinduzi Cup mara baada ya kuinyuka Namungo Fc mabao 2-0.
Simba Sc imefanikiwa kupata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji wake Meddie Kagere pamoja na kiungo mshambuliaji wao raia wa Senegal Sakho ambaye ameonesha kuimarika kwa mechi za hivi karibuni.
Simba Sc rasmi itakutana na Azam Fc fainali ya Mapinduzi Cup ikiwa Azam Fc kufanikiwa kuwaondoa Yanga Sc kwa mikwaju ya Penati.