Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga (kushoto) akiwatambulisha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah H. Mitawa kwa wakurugenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais walipowasili katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino leo Januari 10, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rasi (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wakati wa kikao cha kuwapokea Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah H. Mitawa na kuwatambulisha kwa Menejimenti ya Ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rasi (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wakati wa kikao cha kuwapokea Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah H. Mitawa na kuwatambulisha kwa Menejimenti ya Ofisi hiyo leo Januari 10, 2022 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah H. Mitawa (katikati) akizungumza wakati wa kikao na Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais leo Januari 10, 2022 katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Ignas Chuwa.
*********************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema Ofisi yake imefanikiwa kutatua changamoto za Muungano 11 kati ya 18 zizokuwa zimesalia ndani ya kipindi kifupi na lengo ni kuongeza kasi katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizosalia.
Dkt Jafo ameyasema hayo leo Januari 10, 2022 wakati wa hafla fupi ya kuwakarisha viongozi walioteuliwa kuongoza Ofisi ya Makamu wa Rais na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni wakiwemo Naibu Waziri Mhe. Khamis Khamis na Naibu Katibu Mkuu – Muungano Bw. Abdallah Mitawi.
“Mwaka 2006 ilianzishwa Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano, kikao ambacho huhusisha Makatibu Wakuu na Mawaziri wa pande zote za Muungano na kuongozwa na Mhe. Makamu wa Rais, kikao hiki ni muhimu sana katika kuzipatia ufumbuzi changamoto za Muungano” Jafo alisisitiza.
Amesema kwa upande wa Mazingira Ofisi yake imefanya marekebisho ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 ambayo imejumuisha masuala mtambuka ambayo hayakuwepo kwenye Sera ya Mwaka 1997 na kutolea mfano wa masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi.
“Sera ya Mazingira ya mwaka 1997 ilipelekea kutungwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake ambazo ni msingi katika usimamizi wa Mazingira nchini” Jafo alifafanua.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis H. Khamis na Naibu Katibu Mkuu – Muungano kwa pamoja wameahidi kufanya kazi kwa bidii katika kuendeleza agenda ya maendeleo endelevu, katika kuimarisha Muungano na kusimamia mazingira kikamilifu.