WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akikagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma wakati wa ziara iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma wakati wa ziara iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
Naibu Kamanda wa Operesheni Suma JKT, Meja Goefrey Ngole,akielezea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma
Muonekano wa ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akisikiliza taarifa ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma ikisomwa na Mhandisi Mkazi wa Mradi Aliki Nziku,wakati wa ziara ya Waziri wa kukagua ujenzi wa chuo hicho leo Januari 8,2022.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akikagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma wakati wa ziara yake iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akitoa maelezo kwa Mhandisi Mkazi wa Mradi Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akimsikiliza Mhandisi Mkazi wa Mradi Aliki Nziku,wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
Mkadiriaji ujenzi Mkandarsi John Kyara,akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako,kumaliza kukagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma iliyofanyika leo Januari 8,2022 .
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma kinachojengwa eneo la Nala jijini Dodoma wakiendelea na ujenzi huo.
………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya mfano inayojengwa eneo la Iyumbu jijini Dodoma huku akisisitiza kukamilika kwa wakati.
Akikagua leo Januari 8,2022 maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo inayojengwa na Suma JKT kwa gharama ya Sh.Bilioni 17, Prof.Ndalichako, amesema ujenzi ulianza Julai 2020 na mkataba wa ujenzi ulikuwa miezi 18 na ilipaswa kukamilika ifikapo februari 2022 lakini kasi ya ujenzi hairidhishi kwa kuwa wamebakisha mwezi mmoja kukamilisha lakini bado asilimia 45 ya kazi.
“Kuna kazi nyingi hazijafanyika ukiangalia ghorofa la kwanza bado halijaanza kabisa kuwekwa tofali, kuna kazi za nje kutengeneza viwanja, kufanya landscaping bado zote hazijafanyika na muda wa kazi umebaki mwezi mmoja kwa kweli sijaridhishwa na kasi ya utendaji wa kazi sababu hii ni shule nzuri tulitaka watoto wa kitanzania wapate elimu bora katika mazingira yaliyobora,”amesema.
Amebainisha kuwa walitarajia shule hiyo ipokee wanafunzi wa kidato cha kwanza 2022 lakini kwa hali iliyopo wanahitaji miezi sita mingine hadi Agosti 2022 ili kukamilisha kazi hiyo.
“Nitoe wito kwao Suma JKT kuchukulie hii kazi serious kwa kuwa Mheshimiwa Rais katika vipaumbele vyake ni elimu na hata fedha za UVIKO-19 zilivyopatikana moja ya maeneo yaliyopewa kipaumbele ni ujenzi wa madarasa, fedha zimetoka mwezi Oktoba 2021 madarasa 15,000 yamejengwa na kukamilika kwa asilimia 95 lakini mradi ulioanza Julai 2020 utekelezaji wake upo asilimia 55.”amesema
Waziri Ndalichako amesema hali hiyo haiendani na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan na kutoa wito kwao kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo.
Awali akitoa taarifa ya Mradi huo Naibu Kamanda wa Operesheni Suma JKT, Meja Goefrey Ngole amesema Ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 55 ambapo mabweni ni asilimia 60, bwalo asilimia 85, nyumba za walimu pia ni asilimia 85.
Meja Ngole amesema kuwa gharama za ujenzi huo ni Shilingi bilioni 17.1 ambapo mpaka sasa tayari fedha za matumizi walizopata ni bilioni 7.5.
“Sababu za kuchelewesha mradi umetokana na uzalishaji wa malighafi kama saruji, nondo, ulisuasua na hivyo kuchelewa kupata kwa wakati, kwa maelekezo ya Waziri tutajitajidi kukamilisha na tumeomba kuongezewa muda,”amesema.
Aidha Meja Ngole ameahidi kuzingatia maelekezo ya Waziri na kukamilisha mradi.
Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ametembelea na kukagua ujenzi wa chuo cha Ufundi Dodoma amesema kuwa ameridhishwa na Ujenzi huku akiwasisitiza kuendelea na kasi hiyo ili wamalize kwa wakati .
Prof.Ndalichako amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wanatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa wanafunzi watakaojiunga na chuo hiko.
Naye Mkadiriaji majengo Mkandarsi John Kyara amesema kuwa mpaka sasa Ujenzi umekamilika kwa asilimia 30 na wako ndani ya muda. na thamani ya jengo sh bil 17.
‘Utekelezaji uko vizuri ubora wa kazi uko sahihi na wanaamini mradi utakamilika kwa wakati.”Amesema Mhandisi Kyara