****************************
Na John Walter-Kiteto
Maafisa maendeleo ya jamii nchini wametakiwa kuhakikisha vikundi wanavyoviunda na kuvipatia mikopo vinakuwa na tija kwa kuhakikisha vinafikia malengo tarajiwa.
Hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu ofisi ya waziri Mkuu Kaspar Mmuya wakati akifunga mafunzo ya ujuzi tepe kwa vijana 86 toka kata kumi na moja katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Edward Ole Lekaita kwa kushirikia na ofisi ya waziri mkuu ambapo naibu katibu mkuu huyo ametaka kila halmashauri hapa nchini kuwa na vikundi vya mfano ambavyo vinaweza kunufaisha jamii na kuwa na tija.
Aidha amemshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kuona fursa hiyo ya kuwapatia mafunzo vijana hao ambapo amewasihi vijana hao kutumia vyema fursa hiyo.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi idara ya maendeleo ya jamii ya vijana Julias Twonesha amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha vijana hao juu kuona fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi na kibiashara na usimamizi wa biashara ambapo sasa vijana hao wapo tayari kuingia kwenye soko la kujiajiri wao wenyewe.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Kiteto Roderick kidenya amesema hadi sasa halmashauri hiyo imeshatoa mikopo zaidi ya milioni 152 zishatolewa.
Lengo la Mafunzo hayo ni kuwafikia vijana zaidi ya elfu 40,000 hapa nchini ambao watajengewa uwezo.
Kwa upande mwingine ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kiteto linaloongozwa na Mheshimiwa Edward Ole Lekaita imekabidhiwa jukumu la kulea vikundi hivyo.