**************************
KUINGIZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye GWANTWA MWAKAJILA [45] mkazi wa Ikolo wilayani Kyela kwa kosa la kuingiza nchini bidhaa zilizokatazwa ambazo ni pombe kali na vipodozi kutoka nchi jirani ya Malawi.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 05.01.2022 majira ya saa 08:45 asubuhi huko maeneo ya Katumba – Songwe, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya katika msako uliofanyika maeneo hayo na kukutwa akiwa na bidhaa zilizokatazwa kuingizwa nchini ambazo ni pombe aina ya Ice chupa 20, Pombe carerhum chupa 31, pombe zikomo chupa 14 na vipodozi Epiderm piece 20, Cocopulp piece 12 na Extra clair piece 01.
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili JONAH JACKSON [29] na NEEMA NESTORY [23] wote wakazi wa Ihanga wilayani Mbarali kwa kosa la kupatikana na mali mbalimbali za wizi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 05.01.2022 majira ya saa 20:00 usiku huko maeneo ya Ihanga, Kata ya Rujewa, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa baada ya kupekuliwa walikutwa na mali za wizi ambazo ni:-
- Kinanda 01 aina ya Yamaha,
- Computer 01 aina ya Dell,
- Sound cut 01 aina ya Tasacan,
- Charge 01 ya kinanda na
- Microphone 01 aina ya Samsung mali za JACKOB MWENDA mkazi wa Ihanga.
Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika na tukio hilo na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia 1. HEAVY MUSSA [28] Mkazi wa Ihanga 2. AUGUSTINE MWAKUGA [26] Mkazi wa Ihanga na 3. ANOLD TENGE SAMSON [27] Mkazi wa Iganjo kwa kosa la kupatikana na mali za wizi.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 06.01.2022 majira ya saa 23:00 usiku huko maeneo ya Iganzo, Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri tukio la wizi uliotokea Hospitali ya Igawilo.
Watuhumiwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwao walikutwa na:-
- Madirisha ya shata 16 na vioo vyake,
- Box 10 za marumaru na cutting za marumaru box 02,
- Rangi ndoo lita 1.5 ambavyo thamani yake bado haijafahamika.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ATUGANILE MWAKALOBO [52] Mkazi wa Kijiji cha Katumba kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi @ Gongo ujazo wa lita 21 kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 06.01.2022 majira ya saa 13:52 mchana huko Kijiji cha Katumba, Kata ya Ibighi, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya akiwa anaiuza Pombe hiyo haramu kwenye kilabu chake cha pombe za kienyeji kilichopo Katumba.
KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ANYESHI BATON [50] Mkazi wa Kyimo kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi @ Gongo kiasi cha lita 04 kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 06.01.2022 majira ya saa 11:35 asubuhi huko Kijiji na Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya akiwa anaiuza Pombe hiyo haramu kwenye kilabu chake cha pombe za kienyeji kilichopo Kyimo.