WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea katika mchezo huo dhidi ya timu ya kocha wao wa zamani, Antonio Conte yalifungwa na Kai Havertz dakika ya tano na Ben Davies aliyejifunga dakika ya 34.
Timu hizo zitarudiana Januari 12 Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Arsenal na Liverpool katika fainali ya Carabao 2022.