Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Atupokile Elia akitoa mada kuhusu fursa za Uwezeshaji wa vijana kiuchumi kitaifa katika mafunzo ya Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa vijana yaliyofanyika katika kituo cha Elimu kwa Jamii Kibaya Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara.
Sehemu ya vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mafunzo hayo ya Ujasirimali na Usimamizi wa Biashara yaliyofanyika katika kituo cha Elimu kwa Jamii Kibaya wilayani Kiteto, Mkoani Manyara.
Afisa Uendelezaji Biashara Mwandamizi kutoka Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Bw. Joseph Mwingira akieleza jambo kuhusu masuala ya Ujasiriamali, Ubunifu na Uvumbuzi wakati wa mafunzo hayo.
Meneja kutoka Benki ya CRDB Kiteto, Bi. Gloria Samu akielezea fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo katika kuwezesha vijana.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Amina Sanga akitoa mada kuhusiana stadi za uongozi wakati wa mafunzo ya ujuzi tepe (soft skills) yaliyotolewa kwa vijana kuhusu Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara wilayani Kiteto, Mkoani Manyara.
Kijana Bejamin Darabe (kushoto aliyesimama) akichangia jambo wakati wa mafunzo ya ujuzi tepe (soft skills) yaliyotolewa kwa vijana kuhusu Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara wilayani Kiteto, Mkoani Manyara.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU