Washindi wa zawadi za promosheni ya “Show Love,Tule Shangwe” wakiwa na zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Manyema Mbuyuni wilayani Moshi, jumla ya Tv sita za kisasa na simu janja kumi zilitolewa kwa wapendanao huku pia washindi wa pesa taslimu nao walikabidhiwa pesa walizoshida. Ili ushinde mteja unatakiwa kununua bando na kutumia huduma ya M-pesa kwa kupiga *149*01#
**************************
- Ni gari la kwanza la mshindi wa promosheni ya Tusua Mapene
- Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa washindi wa promosheni ya “Show Love, Tule Shangwe”
Moshi, 30 Disemba 2021 – Kampuni ya teknolojia na Mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa msimu wa furaha unaoitwa “Show Love, Tule Shangwe” pamoja na mshindi mkuu wa kwanza wa shindano la “Tusua Mapene” aliyejishindia gari jipya.
Shindano la “Tusua Mapene” liko katika msimu wake wa nne ambapo zawadi zenye thamani ya Shilingi 2.4 bilioni zitatolewa kwa washindi zaidi ya 300,000. Tangu msimu wa kwanza wa shindano hili, zaidi ya Shilingi 4.8 bilioni zimeshatolewa. Kwa mara ya kwanza magari mapya manne yanakuwa mojawapo ya zawadi zinazoshindaniwa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya gari na zawadi mbalimbali kwa Washindi, Mkuu wa mauzo wa Kanda ya Kaskazini George Venanty alisema, “Leo hii, tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya kabisa kwa kushiriki katika shindano letu la ‘Tusua Mapene’. Tumeona itakuwa vizuri ikiwa zawadi hii ya gari ikakabidhiwa wakati tukiwa tunaendeleza msimu wa upendo na kampeni yetu ya “Show Love, Tule Shangwe” kampeni yenye lengo la kurudisha tabasamu kwa wateja wa kampuni hiyo.
Kampeni ya “Show Love, Tule Shangwe” inalenga kuwapa watumiaji fursa kujishindia zawadi kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na televisheni za kisasa (Smart TV), simujanja na pesa taslimu. Zaidi ya hilo, ili kuendana na msimu wa upendo, zawadi hizi zinagawiwa pia kwa wapendwa ama wenza wa washiriki. Katika tukio hili la makabidhiano, televisheni za kisasa 6, simujanja 10 na zawadi za pesa taslimu pia zilikabidhiwa kwa washindi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai, Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini, Abbas Kayanda alisema, “Bwana Shemmy Malima Chisumo, unavyochukua gari lako, ninakuasa kutumia zawadi hii ambayo ni fursa adimu, uitumie kupiga hatua kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako. Hii iwe hatua ya kwanza kwako, na uendelee kuweka bidii ili uendelee kupanda zaidi kimaisha.”
Kwa upande wake, Bwana Chisumo aliishukuru kampuni ya Vodacom, na kuwasihi wateja kushiriki shindano la Tusua Mapene, lakini pia wasambaze upendo kwa wapendwa wao ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa katika msimu huu wa Sikukuu.
Ili Kushiriki “Tusua Mapene”, mtumiaji anaweza kutuma ujumbe mfupi wenye herufi ‘V’ kwenda namba 15544 au kwa kutumia menu ya USSD kwa kupiga namba *149*01*01# na kuchagua vifurushi husika au vilevile kwa kupitia M-Pesa kwa kupiga namba *150*00# na kuchagua 3 kisha 6 na kuchagua kifurushi anachokihitaji.
Ili kushiriki na kusambaza upendo wa “Show Love, Tule Shangwe”, mteja atapiga *149*01# au atatumia App ya M-Pesa, ataingiza kitu anachokipenda huku akiambatisha na namba za simu za ndugu, jamaa au marafiki anaotaka kugawana nao zawadi iawpo atashinda.
Kuhusu Vodacom Tanzania PLC
Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya huduma za mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi wa data nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa watumiaji zaidi ya milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni zake ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inamilikiwa na Vodafone Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA