TIMU ya Yanga Princess imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya JKT Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao yote ya Yanga Princess yamefungwa na mshambuliaji nyota na chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Aisha Masaka ‘Aisha Magoal’ dakika za 35,38 na 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Yanga Princess inapanda kileleni japo kwa muda, ikifikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Simba Queens ambao hata hivyo wamecheza mechi mbili.