Mtangazaji wa AZAM TV Ahmed Ally leo Jumatatu Januari 3,2022 ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Afisa Habari) katika Klabu ya Simba SC.
Kupitia ukurasa wa Facebook wa Simba SC wameandika
“Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.
Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano. #NguvuMoja