Mratibu taifa wa Shirika la Ulingo Tanzani ( TWCP) Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam katika kikao cha kumaliza mwaka cha Jumuiya hiyo kikiwa na lengo la kushirikishana masuala ya Msingi ya Shirika la Ulingo wanayashughulikia.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Shirika la Ulingo Tanzania ( TWCP) ambalo linaundwa na Jumuiya za Wanawake wa vyama siasa hapa nchini wamemtaka Mbunge wa Kongwa mkoani Dodoma ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuomba radhi kutokana na maeneo ambayo ameyaongea hivi karibuni.
Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha kumaliza mwaka cha Jumuiya hiyo kikiwa na lengo la kushirikishana masuala ya Msingi ya Shirika la Ulingo wanayashughulikia.
Akitoa tamko hilo Mratibu taifa wa Shirika la Ulingo Tanzani ( TWCP) Dkt. Ave Maria Semakafu amesema katika kipindi kifupi wamebaini uwepo masuala ya unyanyasaji wa Viongozi wanawake katika ngazi za maamuzi .
Aidha Semakafu amesema katu kupitia Jumuiya ya Ulingo hawawezi kupuuza utamaduni wa unyanyasaji na Unyanyapaa dhidi ya Viongozi wanawake na badala yake watakemea kwa nguvu zote ili kulinda kizazi cha watoto wa kike wanaokuwa.
Kwa upande wake mwenyekiti taifa wa Shirika la Ulingo Tanzania Mama Anna Magreth Abdallah akizungumza kwa njia ya simu katika Mkutano huo amesema Kitendo cha Mbunge wa Konga Job Ndugai ambaye ni Spika Bunge kusema Mama ameenda kukopa ni kitendo cha Kumvunjia heshima Rais na kuwanjia heshima wanawake wote hapa nchini .
Shirika la Ulingo Tanzania ( TWCP) limekuwa likitekeleza agizo la usawa na katika uongozi wa Kisiasa Tanzania kwa ujumla pamoja na kushughulikia manyanyaso na manyanyapaa mbali mbali ambayo yanatengeneza taswira ya Tanzania ikaonekana inaunyanyasaji katika Demokrasia yake.