****************************
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la polisi Mkoani Pwani, limeeleza katika kumaliza mwaka 2021 kulikuwa na makosa ya jinai 1,756 ambapo mwaka 2020 yalikuwa 1,806 hivyo kufanikiwa kupunguza makosa ya aina hiyo .
Aidha kwa makosa ya usalama barabarani kulikuwa na ajali 58 kwa mwaka 2020 na kusababisha vifo 59 pamoja na majeruhi 67,huku mwaka 2021 ajali zimetokea 47 zilizosababisha vifo 30 na majeruhi 63.
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alitoa ripoti hiyo ya mwaka 2021 alisema wamefanikiwa kupunguza makosa ya jinai na kufikia 50 na wamezuia ajali 11.
Pamoja na hayo, aliwataka madereva kuwa waangalifu na kufuata sheria za usalama barabarani hasa kipindi hiki Cha sikukuu.
Jeshi Hilo ,pia linafanya msako dhidi ya watu watano wanaotumia gari Sienta linalokuja Mjini Kibaha na kufanya utapeli wa fedha kutoka kwa wafanyabiashara wa miamala ya fedha..
“Wahanga wa matukio haya Kama matatu hivi ,yanayotendwa na wahalifu hawa wamedai kutishiwa na silaha ndogo Pisto”
Wankyo Alitoa rai kwa wafanyabiashara hao, kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu hao na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola endapo watawabaini ama wafunge CCTV camera katika maeneo yao ya biashara.
Katika tukio jingine,huko Mlandizi A ,mtaa wa Said Domo polisi imemkamata mtuhumiwa sugu aliyekuwa anatafutwa kwa kufanya matukio ya uvunjaji na uporaji pikipiki Rashid Shaban (24), ambae amekamatwa na kupekuliwa.
Rashid amekutwa na pikipiki moja MC 613 CGA aina ya Haojue rangi nyeusi,vifaa vya kuvunjia kufanya uhalifu,simu za mkononi mbili na vitambulisho mbalimbali vya Edward Joseph Chiwale.