Kufuatia taarifa inayozunguka kwenye Vyombo vya Habari na mitandao ya Kijamii kuhusu baadhi ya wagonjwa kutohudumiwa ipasavyo na watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala iliyoko Jijini Dar es Salaam, Wizara imeyaelekeza Mabaraza ya kitaaluma yafike katika hospitali hiyo na kufanya ufuatiliaji ili kubaini ukweli wa taarifa hizo kisha kuchukua hatua stahiki.
Aidha,taarifa hiyo iwasilishwe Wizara ya Afya, tarehe 02 Januari,2022,saa saba kamili mchana.