Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Mwl Kizito Bahati Sosho akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wengine wakishuhudia mashindano ya Manji Ng’ombe Cup
Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Mwl Kizito Bahati Sosho akisalimiana na wachezaji wa timu ya vijana wa Gedeli Nyakato
fisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela Mwl Kizito Bahati Sosho akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mashindano ya vijana kuanzia umri wa miaka 18 Manji Ng’ombe Cup katika viwanja vya Gedeli
****************************
Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika kuhakikisha inaendeleza na kuibua vipaji vipya vya michezo mbalimbali Kwa watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka kumi na nane na vijana.
Hayo yamesemwa na Kizito Bahati Sosho Afisa Michezo wa Manispaa ya Ilemela akimuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Mhe Hassan Elias Masalla wakati wa kufungua mashindano ya michezo kwa vijana na kufunga ya watoto chini ya miaka kumi na nane yanayojulikana kama Manji Ng’ombe Cup katika viwanja vya shule ya msingi Gedeli kata ya Nyakato ambapo amefafanua Serikali imekuwa na mikakati endelevu katika kukuza vipaji vya watoto wadogo na vijana ikiwemo kuruhusu michezo mashuleni na kuendesha mashindo kama UMITASHUMTA na UMISETA yanayotoa fursa ya kuibua vipaji kwa vijana hasa wanafunzi huku akimpongeza muanzilishi wa mashindano hayo na kumuahidi ushirikiano
‘.. Sisi tupo teyari kushirikiana na wadau kama hawa kina Manji wa Nyakato, tunaamini kupitia mashindano wanayoyaanzisha yatasaidia vijana wetu na taifa..’ Alisema
Aidha Mwalimu Kizito amewataka wadau wengine kujitokeza na kuiga mfano huo kwa kusaidiana na Serikali kuibua vipaji vipya na kuendeleza vilivyopo kupitia mashindano mbalimbali watakayoyaanzisha huku msisitizo ukiwa katika kufuata sheria na taratibu
Kwa upande wake Muanzilishi wa mashindano ya Manji Ng’ombe Cup Bwana Charles Manji amefafanua kuwa Lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa Kwa vijana kuonyesha vipaji vyao huku mshindi wa jumla wa mashindano hayo akiahidiwa zawadi ya Ng’ombe na wengine wakiwania mbuzi, jezi na vikombe
Paschal Masanja ni Moja ya washiriki wa mashindano hayo kutoka timu ya watoto akishukuru Kwa uwepo wa mashindano hayo kwani mbali na kuibua vipaji vyao yamewafanya wasijikite katika makundi maovu ya wizi na matumizi ya dawa za kulevya.