NA MUSSA KHALID
Aliyewahi kuwa Diwani wa Kata ya Kijichi Manispaa
ya Temeke jijini Dar es salaam Elias Mtarawanje ameshinda kesi iliyochukua takriban miaka
miwili iliyokuwa inamkabili ya tuhuma za kupokea rushwa kwa nyakati tofauti na
hivyo kuachiwa huru.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es salaam Wakili Dkt Aloys Rugazia ambaye
amesimamia shauri la Mtarawanje ambalo limekuwa linasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke
amesema kesi hiyo NO,266 ya mwaka 2020 ilikuwa ni tuhuma na hivyo Mahakama imewabaini
kuwa hawana hatia.
Dkt
Rugazia amesema hiyo imemaanisha kuwa kiwango cha fedha kinachosadikiwa mteja
wake kuchukua hakikua na uthibitisho wowote wa kuwa pesa hizo ambazo
zimepelekwa mahakamani kama ushahidi hivyo mahakama ikaamua kutupilia mbali
shauri la upande wa Mwendesha Mashtaka na kumuachia huru Diwani mstaafu
Mtarawanje.
‘Tunashukuru
sana Taasisi ya Kupambana na Rushwa PCCB kwani tumeweza kupata dhamana bila
usumbufu wowote na baada ya kufikishwa mahakamani ushahidi wa pande zote
ulichukuliwa na wateja wetu wawili Bwana Elias Mtarawanje na Constantin Moris
walibainika kwamba hawana kosa’amesema Wakili Dkt Rugazia
Aidha
Wakili Dkt Rugazia amesema umuhimu wa Kesi hiyo imetokana na Mtarawanje kuwa
diwani kijana kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hivyo tuhuma dhidi
yake zimeleta msisimko kwa jamii kutaka kufahamu hitimisho lake.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Temeke Mohammed Abdalah
amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa haki imetendeka kwani Mtarawanje alikuwa
kiongozi shupavu ambaye amefanya kazi yake kwa uaminifu bila ya uoga.
‘Kama
chama kina taratibu zake na miongozo yake lakini ni jambo zuri kwa Mwanachama
mwenzetu aliyekuwa Diwani kushinda hivyo ninayofuraha ya kuona kijana mwenzangu
amepata haki yake na ukweli umedhihiri’amesema Mohammed
Amesema
kuwa kwenye siasa kuna changamoto nyingi pindi vijana wanavyofanya mambo mazuri
wengine wanaingiwa na wivu kwani Mtarawanje alipambana sana katika ujenzi wa
Mradi wa barabara zilizokuwa chini ya DMPD.
Ikumbukwe
kuwa Diwani huyo mstaafu wa Kata ya Kijichi alifikishwa mahakamani na kusomewa
mashtaka yake na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa TAKUKURU,Mwanakombo Rajabu mbele
ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Catherine Madili.