Raja walitangulia kwa bao la kujifunga la beki Yasser Ibrahim dakika ya 13, kabla ya Mohamed Taher kuisawazishia Ahly dakika ya 90 na hakukuwa na bao katika dakika 30 za nyongeza hadi mikwaju ya penalti ilipoamua mshindi.
Katika mikwaju ya penalti, kila timu ilipata tano zote za mwanzo, Ali Maaloul, Badr Benoun, Percy Tau, Ahmed Radwan na Taher wakiifungia Ahly na Mohamed Azrida, Zakaria El Wardi, Marouane Hadhoudi, Mahmoud Benhalib na Nahodha, Mohsine Mouataouali wakiifungia Raja.
Kwenye ‘Penalti za Kifo’ Akram Tawfik alifunga ya Ahly, lakini Madkour akapaisha ya Raja, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na kuibua shangwe kwa mashabiki waliosafiri kutoka Misri.