…………………………………………………………..
KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYAA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama limejipanga vyema kuhakikisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya zinasheherekewa kwa amani na utulivu katika maeneo yote ya Jiji na Mkoa wa Mwanza. Hivyo tuwatoe hofu Wananchi na wageni wanaotembelea Mkoa wetu kwamba ulinzi umeimarishwa wa wao na mali zao.
Aidha katika kuhakikisha uhalifu wa aina zote unadhibitiwa, askari watakua wanapita katika maeneo mbalimbali wakiwa kwenye doria za miguu, pikipiki na magari huku wakiwa na Mbwa wa Polisi, hivyo tuwatake wananchi wanapowaona watoe ushirikiano kwa askari wetu kwa kuwapa taarifa za uhalifu au taarifa zozote zenye viashiria vya uhalifu ili uweze kudhibitiwa mapema kabla haujatendeka.
Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza litahakikisha Nyumba zote za ibada, kumbi za starehe na maeneo mengine ulinzi unaimarishwa vyakutosha kwani askari watakua katika doria za miguu. Pia tuwatake wanachi wanaokwenda kwenye mikesha katika sikukuu hizi wasiache nyumba zao bila uangalizi wa walinzi/mlinzi kwani kunaweza kushawishi wezi kuiba.
Vilevile tuwakumbushe wazazi na walezi kuwa Pamoja na kusherekea sikukuu hizi wasisahau majukumu yao kuwa makini na watoto wao kwa kutowaacha peke yao barabarani na katika sehemu za michezo mfano maeneo ya beach/mialo na kwenye bembea. Pia nimarufuku kwa madereva wa vyombo vya moto kuendesha wakiwa wamelewa au mwendo kasi, endapo ikibainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Hata hivyo kwa wale wenye tabia za kuchoma matairi barabarani waache kwani ni kosa kisheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawatakiwa wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza na Watanzania kwa ujumla sikukuu njema ya Krismasi na Mwaka Mpya. Lakini pia kusheherekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.
IMETOLEWA NA;
Ramadhan Ng’anzi – SACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA