Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao cha kupata mrejesho kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Ofisi ya waziri Mkuu,Sera,Bunge,Uratibu,Kazi,Vijana na wenye Ulemavu imesema imepunguza muda wa maombi ya kibali cha maombi ya kazi kwa raia wa kigeni kutoka siku 35 mpaka kufikia siku moja hadi saba.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Kazi (Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, Bunge ,Uratibu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ) Brigadia Jenerali Frances Ronald Mbindi wakati wa kikao cha kupata mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu matumizi ya Mfumo wa kushughulikia Maombi ya Vibali vya Kazi kwa Raia wa Kigeni kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
“Iwapo muombaji atakamilisha mambo yake yote vizuri ni masaa au siku moja atapata kibali cha kazi lakini ‘maximum’ ni siku saba ukilinganisha na zamani walitumia siku 14 na zaidi,” Amesema.
Aidha amesema mfumo huo wa matumizi ya njia za kielektroniki katika uchakataji wa maombi ya vibali ulianza rasmi Aprili 23, mwaka huu.
Amesema kwamba utaratibu wa awali ulimlazimu muombaji wa kibali hicho kupitia hatua 33 hadi kupata kibali, huku serikalini napo kukiwa na michakato mingi ya kujaza karatasi, lakini sasa hilo halipo.
Kwa upande wake, Mdau wa vibali vya kazi kutoka Kampuni ya Reco Engineering & Multicable Ltd, Aboubakar Mkadam, amesema mfumo wa zamani wa uombaji vibali hivyo ulikuwa na changamoto nyingi.
“Mfumo wa zamani ulipoteza muda mwingi, gharama kubwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma lakini huu wa kielektroniki umerahisisha muda kwa kuwa nyaraka ikitakiwa unaiweka mtandaoni ndani ya dakika moja inafika,” Amesema.