Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akiwa na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wakitembelea na Kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO-19 ziara hiyo imefanyika leo Desemba 22,2021
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akitoa maelekezo mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari za Miyuji,Umonga,Kiwanja cha ndege,Viwandani,Itega na Dodoma Sekondari yanayojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO-19 ziara hiyo imefanyika leo Desemba 22,2021
Mkuu wa wilaya wa Dodoma,Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO-19 ziara hiyo imefanyika leo Desemba 22,2021
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Joseph Mafuru,akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO-19 ziara hiyo imefanyika leo Desemba 22,2021
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa kutumia fedha za UVIKO-19 ziara hiyo imefanyika leo Desemba 22,2021
…………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kupitia fedha za mapambano dhidi ya UVIKO- 19 ambapo Mkoa huo unatarajia kukabidhi madarasa 601 Desemba 30 mwaka huu.
Hayo ameyasema leo Desemba 22,2021 jijini Dodoma mara baada ya kufanya ziara pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari.
Mtaka amesema kuwa ujenzi wa madarasa unakwenda vizuri na matarajio ya mkoa ni kukabidhi vyumba vyote vya madarasa ifikapo Desemba 30 mwaka huu.
“Kama mkoa tumeridhika na hatua ya ujenzi ilipofikia na tunataraji kufanya hafla kukabidi vyumba hivi 601 vya mkoa katika wilaya moja ambayo tutaichagua kwa niaba ya mkoa”amesema
Aidha Mtaka ameziagiza wilaya zote ambazo zinatekeleza mradi huo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kuhakikisha kuwa zinapanda miti katika maeneo ya shule.
“Wakati madarasa haya yanajengwa naomba yaendani na zoezi la upandaji wa miti haiwezakani shuke inakuwa na majengo mazuri lakini maeneo yake yamepauka lazima kila mwanafunzi apate mti mmoja wa kuutunza”amesema Mtaka
Hata hivyo Mtaka amewataka wazazi na walenzi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza kuhakikisha ifikapo Januari 17 Mwaka2022 watoto wote wawepo shuleni.
“Itakuwa ni aibu kubwa kuwa na majengo mazuri na ya kisasa ambayo yanajitosheleza lakini watoto hawaendi shule, hatutaki kuona watoto wanaonekana sokoni, mitaani pamoja na mashambani au kuwa sehemu ya kutunza familia” amesisitiza Mtaka
Pia ameutaka Uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha unakamilisa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wakati ili watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza waweze kusoma.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Dodoma Dk. Fatma Mganga, amesema kuw ujenzi wa vyumba vya madarasa 601 unagharimu kiasi cha Sh. bilioni 12.02.
Dk.Mganga amesema kuwa pamoja na ujenzi wa madarasa hayo 601 ya shule za sekondari lakini pia mkoa wa Dodoma unajenga madarasa 175 kwa ajili ya shule shikizi ambayo yataghalimu kiasi cha Sh.bilioni 3.5.
Awali Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru ameihakikishia Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dodoma kuwa hadi ifikapo Disemba 24 Mwaka huu watakabidhi Madarasa hayo.
“Sisi kama Jiji tunajitahidi katika kutekeleza Mradi huuu na tunamshukuru Sana mheshimiwa Rais kuona umuhimu wa watoto ambao walikuwa wanakosa nafasi kuweza kusoma,”amesema