Muhanga aliyoeka Fedha zake katika Kampuni ya Masterlife, kwa upande wa Mkoa wa Mjini, Hidaya Haji Mkema akiwaomba Wahanga wenzake kwenda kuchukua Fedha zao bila kutegemea faida, katika Hafla ya zoezi la kuwalipa Wahanga waliyoweka Fedha zao katika Kampuni ya Masterlife lililofanyika Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
Muhanga aliyoeka Fedha zake katika Kampuni ya Masterlife, kwa upande wa Mkoa wa Mjini, Omar Hamza Omar, akimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa upendo aliyokuwa nao kwa Wananchi wake,katika Hafla ya zoezi la kuwalipa Wahanga waliyoweka Fedha zao katika Kampuni ya Masterlife lililofanyika Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, wakiwa katika zoezi la kuwalipa Wahanga waliyoweka Fedha zao katika Kampuni ya Masterlife, kwa upande wa Mkoa wa Mjini, Hafla iliyofanyika Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
Baadhi ya Wahanga waliyoweka Fedha zao katika Kampuni ya Masterlife, kwa upande wa Mkoa wa Mjini,wakia katika zoezi la kusubiri kulipwa Fedha zao huko Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
**********************
Na Pili Ali / Maelezo. 21/12/202.
WANANCHI wa Mkoa wa Mjini walioweka fedha katika kampuni ya Masterlife wamesisitizwa kwenda kuchukua fedha zao na sio kupata faida kama walivyotarajia .
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Saumu Khatib Haji, wakati akiwa katika zoezi la ulipaji fedha kwa wahanga waliyoweka Fedha zao katika kampuni hiyo huko skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein.
Amesema fedha wanazolipwa wahanga hao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni zile walizoweka tu na sio faida.
Akifafanua zaidi amesema wananchi wanaohusika kwenda kuchukua fedha hizo ni wale ambao majina yao yalitajwa katika tangazo lililotolewa ndani ya Gazeti la Zanzibar Leo la tarehe 3 na tarehe 4 Disemba .
Aidha amesema kuwa kunachangamoto kwa baadhi ya wahanga kuwawakilisha watu wengine na kutopeleka vielelezo vinavyohitajika ambavyo havijakamilika jambo ambalo linateta usumbufu.
Nao wahanga waliyoeka Fedha zao katika Kampuni ya Masterlife wamemshukuru Rais wa awamu ya nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuwajali wananchi wake na kuchukuwa jukumu la kuwalipa Fedha zao walizoweka na kuhakikisha kila mmoja atanapata haki yake Kama inavyostahiki.
Hivyo wamesema wamekuwa na furaha , na imani ya kweli kwa Rais wao kwani walikuwa mameshakata tamaa yakuzipata fedha zao walizoweka katika Kampuni hiyo.
Zoezi hilo la awamu ya kwanza kwa Mkoa wa Mjini linatarajiwa kumalizika siku ya tareha 24 mwezi huu.