Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora Louis Bura akihutubia walimu , wananchi na wanafunzi wa shule ya Itundu wilayani humo
Mkurugenzi cha uzalishaji wa zao la Tumbaku kutoka kampuni ya Alliance one, David Mayunga akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya Urambo.
Viongozi mbalimbali akiwemo diwani wa kata ya Kapilula na viongozi wandamizi wa kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Alliance one .
Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora Louis Bura akipokea vifaa vya kuchunja maji ya kunywa kwa wanafunzi na walimu wilaya Urambo kutoka kwa kiongozi wa kampuni hiyo ya Korea Tomorrow &Clobal Corporation (KT&G) Seong Hun Jeong.
…………………………………………………………
Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora Louis Bura amewataka viongozi wa vyama vya ushirika wa zao la tumbaku wilayani humo kuwa wawazi katika usimamizi wa shughuli zote za ushirika ili kuepuka vyama hivyo kufa kutokana na madeni yasiyolipika.
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati akipokea vifaa vya kuchujia maji ya kunywa kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Itundu wilayani humo.
Vifaa hivyo vilivyotolewa na kampuni ya ununuzi wa zao la Tumbaku ya alliance one kwa kushirikiana na mteja wa kampuni hiyo ya Korea Tomorrow &Clobal Corporation (KT&G).
Alisema kwamba kutokana na kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa vyma vya msingi vya ushirika kumesababisha baadhi kushindwa kulipa madeni na kufa hali inayoadhiri kilimo cha tumbaku wilayani humo.
Alisema wilaya urambo ndio mkoa kilele kwa uzalishaji wa zao la Taumbaku nchini lakini kutokana na viongozi kutokwa wawazi kumeshabisha vyama kufa kutokana na madeni.
Alisema kwamba wilaya ya Urambo ilikuwa na vyama vya msingi vya ushirika 54 vilivyobakia ni 16 vingine vyote vimekufa kutokana na madeni yasiyilipika lakini kwa sasa vyama.
“ Amcos wamekuwa wakikopeshwa ,mbole na magunia ya kufungia tumbaku na mwisho wanashinda kulipa madeni kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.”alisema Mkuu wa wilaya yaUrambo .
Louis Bura alisema kwamba vyama vya msingi vya ushirika vinapasawa kubadilika kwa kufanya kazi kwa maslahi mapana kwa kufuata ,uadilifu ,uwazi na uwajibikaji kama miongozo ya ushirika inavyotaka.
Naye mkurugenzi cha uzalishaji wa zao la Tumbaku kutoka kampuni ya Alliance one, David Mayunga alisema wametoa vifaa hivyo vya kuchujia maji ya kunywa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Itunda wilayani humo.
Alisema kwamba vifaa vipatavyo 943 kwa ajili ya shule 224 vikiwa na thamani ya shilingi million 283,182,900 kwenye maeneo wanayonunua zao la tumbaku ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida kwa jamii.
Alisema kwamba licha ya kutoa maeneo hayo wilaya ya urambo pekee nitapokea vifaa hivyo 54 kwa ajili ya shule za msingi 13 vikiwa na thamani ya shilingi milioni 16,216,200.
Mayungu alisema kwamba kutoa vifaa hivyo vya kuchunja maji ya kunywa vitaimarisha juhudi za serikali na wadau wengine kuhakikisha Afya za wanafunzi na walimu zinakuwa bora.
Alisema ari ya ufundishaji kwa walimu na mahudhurio shule kwa wanafunzi yataongezeka .
Mratibu utumikishwaji Watoto katika mashamba ya tumbaku Tanzania kutoka Alliance one Laurence Safari alisema kwamba kutolewa kwa vifaa hivyo kutapunguza utoro kwa wanafunzi na kuongeza madhurio mashuleni.
Mwalimu mkuu shule ya msingi Itundu Grace Mombo aliishukuru kampuni hiyo ya ununuzi wa za zao la Tumbaku kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia sana kupunguza homa za matumbo kwa wanafunzi .
Alisema kwamba maji yanoyotumika maendeo mengi ya vijijini sio safi na salama lakini kupatikana kwa vifaa hivyo vya kuchunja maji ya kunywa tatizo hilo litapungua