Muonekano wa gari za kusafirishia taka ngumu
kwaaajili ya kuimarisha usafi zilizozinduliwa na Waziri wa Nchi (OR) Tawala
za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed huko viwanja vya
kumbu kumbu ya mapinduzi Kisonge, chini ya udhamin wa V-CLEAN
wakishirikiana na Baraza la mji zanzibar.*
*Waziri *wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za
SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akikata utepe kuzindua gari za kisasa za
kubebea taka ngumu kwaajili ya kuimarisha usafi ,hafla iliyofanyika viwanja
vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge.*
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara
maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akizindua mifuko maalum ya kuhifadhia
taka laini,taka za matumizi ya majumbani na taaka za mahotelini kwaajili ya
kuimarisha usafi, hafla iliyoandaliwa na V-CLEAN wakishirikiana na Baraza
la Manispaahuko Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.*
*Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara
maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akizindua mifuko maalum ya kuhifadhia
taka laini,taka za matumizi ya majumbani na taaka za mahotelini kwaajili ya
kuimarisha usafi, hafla iliyoandaliwa na V-CLEAN wakishirikiana na Baraza
la Manispaahuko Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.*
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za
SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed watatu kutoka kulia,Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Idrisa Kitwana,mwenyekiti kampuni ya vigor Taufik Turkey wakiwa
na viongozi mbalimbali wa manispaaa , wakionyesha mifuko maalum ya
kuhifadhia taka laini ,taka za matumizi ya nyumbani,na taka za hotelini
,mara baada ya uzinduzi WA mifuko hiyo huko viwanja vya kumbukumbu za
mapinduzi Kisonge Zanzibar.*
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za
SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed akiwa ndani ya moja ya gari alizozizinduwa
kwajili ya kuimarisha usafi kupitia kampuni ya wawekezaji wa V-CLEAN ili
kukagua zaidi gari hiyo,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za
mapinduzi Kisonge.*
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za
SMZ.Mheshimiwa Masoud Ali Mohamed amewataka wananchi kuziunga mkono
jitihada za Serikali katika kuhakikisha mji unakuwa safi.
Kufanya hivyo kutaisaidia Zanzibar kuwa na haiba nzuri ambayo itaweka
ustawi bora na kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka
pamoja na gari za kisasa za kusafirishia zilizotolewa na Kampuni ya
Vigor huko katika Uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge .
Amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mheshimiwa Dkt,Husein Mwinyi ametoa rai yenye dhamira njema
kuhakikisha mji unakuwa safi hivyo iko haja ya wananchi kushirikiana
kwa pamoja kudumisha usafi katika maeneo yao.
Aidha alisema Kampuni ya Vicline itashirikiana na Serikali kuondoa
changamoto iliyopo ya kusambaa taka taka katika mji jambo ambalo
linapoteza haiba na ustawi wa mji .
Alifahamisha suala la kujenga nchi sio la serikali pekee bali ni
jukumu la wananchi wote hivyo iko haja ya mashirikiano ili kuhakikisha
azma iliokusudi inafikiwa.
Waziri Masoud alisema licha ya taka kuna uchafuzi wa mazingira ya
kubandika matangazo mengi kiholela bila ya kufuata utaratibu kufanya
hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa alisema
bado mji haujaridhisha hasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambao ni
jicho la Zanzibar hivyo sheria ndogo ndogo zipitiswa kwa kutoa faini
kwa wanaochafua mji .
Alisema ni vyema jamii kuimarisha mji kwa kupanda bustani mbali mbali
katika maeneo yao ili kuengeza uzuri wa mji wa Zanzibar.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mjini, Ali Khamis alisema Baraza la
Manispaa kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa taka kumetokana
na gharama kubwa ya uendeshaji, uchakavu na uwezo mdogo wa vifaa vya
ukusanyaji wa taka pamoja na uchache wa rasilimali watu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kampuni Vigor ambae pia ni Mbunge wa Jimbo
la Mpendae, Taufik Salum Turkey amesema kampuni hiyo inamkakati wa
kuzisarifu taka kwa lengo la kubuni miradi na kuzalisha viwanda vidogo
vidogo vya vyakula vya kuku majongoo mbolea pamoja na karatasi jambo
ambalo litasaidia kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana.
Akitoa wito kwa jamii alisema usafi ni jukumu la wote hivyo
tushirikiane tuimarishe mji kwa pamoja na Kauli Mbio ya Uzinduzi huo
ni Weka Mji Safi kwa Utalii bora Zanzibar.