…………………………………………………………………….
Na. Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Ujumbe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ukiongozwa na Rashid Maftah umetembelea ,Halmashauri ya Mji Kibaha kuona hatua ya ujenzi wa Madarasa mradi Na.5441-Tanzania Covid-19 Social-Response and Recovery Plan yaliyoanza kujengwa Mwezi Oktoba,2021.
Mkurugenzi wa Mji Kibaha ,Mhandisi Mshamu Munde alisema, haki ya utekelezaji ni nzuri na imezingatia viwango kutokana ushirikishwaji wa kamati ziliundwa kwa kuhusisha wataalam na Wananchi.
Akisoma taarifa Afisa Afisa Mipango,takwimu na ufuatiliaji wa Kibaha Mji Wambura Yamo alisema jumla ya shilingi milioni 940 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kujenga Madarasa 47, tayari kiasi cha milioni 792,612,524.84 kimetumika ambapo Madarasa 17 yamekamilika kwa asilimia 100 na 30 yapo kwenye hatua za mwisho za ukamilisha.
Rashid Maftah alipongeza ushirikiano ulioneshwa na kamati zote zilizopelekea kufikia kiwango cha ujenzi cheji tija huku akifurahishwa na akina Mama ambao wameshiriki kikamilifu kwenye kazi ikiwemo kupaka rangi,kupika chakula na kazi nyingine kwani kando ya mradi kutatua changamoto ya Madarasa lakini ulitoa ajira.
Afisa Mipango wa Mkoa ,Rukhia Muwango aliwashukuru kamati,wajenzi na wasimamizi wa mradi kwani hakuna changamoto kubwa iliyowashinda kutatua na kwamba ilipojitokeza waliweza kuitatua kwa wakati na kazi zinafanyika usiku na Mchana.
Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kibaha Karimu Mtambo na Ramadhani Lutambi walimshukuru Rais Mama Samia Kwa kuikumbuka Kibaha na kwamba kwa kufanya hivyo amewaondoa kwenye mkwamo wa kimasomo Wanafunzi wote wanaotarajia kuanza tarehe 17 Januari,2022 na kwamba wataanza kwa wakati bila kuathiri kalenda yao