Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi zawadi ya mwanafunzi wa MEMKWA ambaye amefanya vizuri kwenye masomo yake
**********************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amesema Serikali haifuraishwi na uwepo wa watu wazima zaidi ya 15 elfu wasiojua kusoma na kuandika Wilayani humo huku akiwahimiza kujiunga na elimu ya watu wazima
Akizungumza katika Hafla ya kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya watu wazima (MEMKWA) alisema idadi hiyo ni kubwa hivyo ni muhimu waratibu wa elimu kuweka mkakati maalum kulisaidia kundi hilo haraka iwezekanavyo
Mkuu huyo wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassani Moyo ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa kupitia Idara ya elimu iliyobainisha kuwa watu wazima wapatao 15 elfu na mia moja Wilayani humo hawajui kusoma na kuandika.
Akisoma risala kwa Mgeni wa Heshima katika kilele za Maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa watu wazima afisa elimu shule ya msingi halmashauri ya wilaya ya Iringa Fusi Hafla hii iliyofanyika katika kata ya Lumuli imebainisha idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika katika wilaya hiyo inayokunikana mkoani Iringa nyanda za juu kusini
Alisema kuwa maeneo mengi ya vijijini wananchi wake wengi hawajui kusoma na kuandika kutokana na mira na tamaduni zao hivyo wananchi wanaopatikana vijijini wanatakiwa kujua umuhimu wa elimu kwa ajili ya manufaa yao.
Fusi alisema kuwa idadi hiyo ni kubwa kulingana na wakati uliopo hivyo wananchi wanatakiwa kutambua na kujua umuhimu wa kupata elimu ya awali ya kujua kusoma na kuandika kwa ajili ya kuwaondolea ujinga ambao utawasaidia kuwakomboa katika harakati za maisha.
Moyo alieeleza namna ambavyo Serikali haifuraishwi na idadi kubwa ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika hivyo wananchi wa Iringa wanatakiwa kuhamasishe watu wazima waendelee kujiunga kwenye elimu ya watu wazima.
Alisema kuwa kumekuwa na utapele mkubwa kwa wananchi ambao wamekuwa hawajui kusoma na kuandika hivyo ni lazima wananchi wengi wa vijijini lazima wapate elimu ya kusoma na kuandika ili waachwe kudanganywa na matapeli.
“Haiwezekani kila siku unapata kesi nyingi za wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa kutapelewa na nimekuwa nafaatilia kwa ukaribu na nimegundua kuwa wengi wao ni wale wananchi ambao hawajui kusoma na kuandika jambo ambalo linachangia kutapeliwa kirahisi tofauti na wale wananchi ambao wanaelimu ya kujua kusoma na kuandika” alisema Moyo
Moyo alitumia jukwaa hilo kuwahimiza waratibu wa elimua ya watu wazima katika wilaya hiyo inayokutikana mkoani Iringa kuchukua hatu kupitia mfumo wa MEMKWA kulisaidia kundi hilo ili liweze kusoma na kuandika
Katika hatua nyingine amewakumbusha wazazi na jamii kwa ujumla kuwekeza katika elimu ikiwemo suala la kuwaaandikisha shule watoto wao kwa muda muafaka
Hafla hiyo iliyowakutanidha viongozi wa Idara ya elimu Wanafunzi na wadau wengine wa elimu ya watu wazima imebeba nara isemayo ELIMU YA WATU WAZIMA KWA MAENDELEO YA TAIFA