Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dk. Fatma Mganga,akizungumza wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu tawala Msaidizi anayeratibu Sekta za Uchumi Mkoa wa Dodoma Bi. Aziza Mumba,akielezea utekelezaji wa mikopo ianyotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Vijana,Wanawake na Watu wenye ulemavu kwa kipindi cha mwaka 2017/18 hadi Novemba 2022 wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe. Tunu Pinda,akizungumzia nafasi ya mwanamke katika uwekezaji wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkurungezi wa Taasisi ya Uongozi Bw.Kadari Singo,akielezea umuhimu wa viongozi kujitambua na kujenga timu zenye tija wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Uendelezaji Biashara kutoka SIDO Bw.Crispin Kapinga,akitoa mada kuhusu jukumu la SIDO katika kukuza na kuboresha shughuli za uzalishaji kwenye viwanda vidogo wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dk. Fatma Mganga,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imetoa Jumla ya Sh. 11,920,750,969 kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri saba za Mkoa wa Dodoma.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dk. Fatma Mganga,wakati akizungumza katika kikao cha Tathimii ya Utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi.
Kikao hicho pia kiliwashirikisha wanawake wajasiriamali, wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo.
Dk.Mganga amesema kuwa fedha hizo zilizotolewa kwenye makundi hayo katika Halmashauri za Bahi, Chamwinio, Chemba, Dodoma Jiji, Kondoa, Kondoa mji, Kongwa na Mpwampwa.
Amesema kuwa Sh. 7,004,724,612 zilielekezwa kwa vikundi vya wanawake, Sh 4,264,231,059 kwa vikundi vya vijana na Sh. 652,795,298 kwa vikundi vya watu wenye ulemavu
” Kutokana na fedha hizo, jumla ya wanawake 12,427 wamenufaika huku wanaume wakiwa ni 2,249.”amesema
Dk. Mganga amesema kuwa wanawake wameonyesha kuwa na ufanisi mkubwa katika kurejesha mikopo ambapo ni asilimia 43, wakifuatiwa na watu wenye ulemavu kwa asilimia 35 na vijana kwa asilimia 28.
Dk. Mganga amesema tathimini inaonesha kuwa fedha zilizotolewa kwenye makundi hayo zimeelekezwa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya viwanda vidogo vya machinjio ya kuku, kukamua Mafuta ya alizeti,mkusaga unga wa sembe, kutengeneza majiko banifu na mama lishe.
“Fedha hizi zilizotolewa kwa vikundi vya wanawake, walemavu na vijana zimesaidia upatikanaji wa mikopo kwa makundi ambayo hayawezi kukopesheka kupitia taasisi za fedha.
“Pia mikopo hii imeleta mafanikio makubwa katika uchumi wa wanawake kwa wanawake wengi kujiajiri, kuboresha maisha yako binafsi wa kuwa wanapata fedha za ziada kupitia biashara zao na kuongeza idadi ya wanawake wanaojiunga na bima ya afya.”amesema
Awali Katibu tawala Msaidizi anayeratibu Sekta za Uchumi Mkoa wa Dodoma Bi. Aziza Mumba amesema pamoja na kuwapo na mafanikio yatokanayo na mikopo hiyo kuna changamoto ya upungufu wa rasilimali watu wenye weledi katika kusimamia utoaji na urejeshaji wa mikopo.
Bi.Mumba amesema kuwa kumekuwapo na changamoto ya upungufu wa rasilimali fedha na vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa mikopo sambamba na kuwapo kwa idadi kubwa ya maombi ya mikopo ikilinganishwa na uwezo wa halmashauri husika jambo linalopaswa kushughulikiwa.
“Ili kuondokana na changamoto hizi Kuna haja ya kila Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ili kuongeza kiasi cha utoaji mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali vinavyoomba mkopo.
Mumba, ameshauri kuwa kuwapo kwa mafunzo ya uongezaji thamani ya mazao na kuunganishwa na mnyororo wa masoko kwa wanavikundi.
“Pia kuna haja ya kuwapo kwa mfumo wa TEHAMA ambao utasaidia kukumbusha waliokopa kurejesha fedha kwa wakati na hatimaye kuwezesha wengine kukopa.”amesema
Kwa upande wa Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe. Tunu Pinda,ameeleza nafasi ya mwanamke katika uwekezaji kiuchumi na kusisitiza kuwa kutokana na wanawake wengi kuelimika na kukubali kuingia kwenye biashara hali zao za maisha zimeimarika.
Amesema kuwa usawa wa kijinsia unaoendelezwa na serikali umesaidia kwa kiasi kikubwa wanawake kujitambua na kukubali kuwezeshana wao kwa wao na kuondokana na dhana ya udhaifu iliyokuwa imezoeleka.
“Wanawake wengi wanaishi kwenye nyumba nzuri,wanasomesha watoto,wanazingatia usalama wa chakula na yote haya yanakuja kutokana na faida ya uwekezaji,kwa ujumla tuko mbele sana kiuchumi Kwa Sasa asilimia 50 ya wanawake wanamiliki akaunti za benki.”
Aidha ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kuendesha biashara zao kwa kutumia mikopo kutoka taasisi za mikopo yenye riba nafuu hali itakayo wakwamua kiuchumi.
“Mimi mwenyewe nimekuwa nikikopa kwenye taasisi mbalimbali na kutumia fedha hizo kwenye masuala ya kilimo biashara na kusaidia kutoa ajira kwa wanawake wengine.”amesema