Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akijadiliana jambo na mweyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa Said Rubeya wakati wa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021
***********************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020 – 2025 kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021.
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Iringa mjini ,Moyo alisema mojawapo ya mafanikio ni utoaji wa mikopo kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu isiyo na riba kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Moyo alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imefanikiwa kusimamia sekta mbalimbali za kiserikali vizuri,kukuza uchumi wa wananchi hasa wakazi wa manispaa ya Iringa,kuimarisha huduma za kijamii kiuchumi yote hiyo inatokana na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020 – 2025.
Alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021 halmashauri ya manispaa ya Iringa imefanikiwa kukuza mapato kwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato hayo.
Moyo alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021 halmashauri ya manispaa ya Iringa imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani na kuanzisha vyanzo vipya ya kukusanya mapato.
Alisema kuwa kwa kipindi hiki jumla ya wanachama 2923 wamejiunga katika bima ya afya kwa ajili ya kupata huduma za kiafya ambazo nazo kwa kiasi kikubwa zimeboreshwa kwa lengo la kupewa kipaumbele cha kupata huduma za afya katika maeneo husika.
Moyo alisema kuwa ili kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya wameanza kujenga kituo kipya cha afya katika kata ya mkimbizi,ukarabati wa zahanati ya Mtalagala iliyopo kata ya Nduli pamoja na umaliziaji wa zahanati ya Itamba iliyopo kata ya Mkwawa
Alisema kuwa uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa imefanikiwa kutibu na kutoa chanjo kwa mifugo na jumla ya mifugo 177304 ikiwa mbuzi 212,ng’ombe 3011, mbwa 2364,kuku 171717 na jumla ya mbwa 215 wameuwawa kwa lengo la kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Moyo alisema kuwa halmashauri inaendelea kuhakikisha huduma ya josho inapatikana kwa wafugaji wote tena kwa ubora unaotakiwa ambapo kunajumla ya majosho nane ambayo yote yapo katika manispaa ya Iringa.
Alisema kwa kipindi cha mwezi wa saba hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021 wamefanikiwa kutoa mikopo ambayo haina riba kwa vikundi 23 ambapo vikundi vya wanawake 11 vijana 7 na watu wenye ulemavu 13 ambapo jumla ya milioni 92 ziligawiwa kwa walengwa hao.
Mara baada ya mkuu wa wilaya huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwampongeza mkuu wa wilaya Mohamed Hassan Moyo kwa kazi kubwa anayifanya ya kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.
Rubeya alisema kuwa manispaa ya Iringa imeanza kupiga hatua za kimaendeleo kwa kasi kubwa mara baada ya kuteuliwa kwake kuwa kiongozi wa wilaya hiyo kwa kuanza kutatua changamoto za wananchi ambazo zimekuwa kero za wananchi kwa kipindi kirefu.
Alisema kuwa amefanikiwa kuinganisha vilivyo serikali na chama kuwa kitu kimoja ambapo wanafanya kazi kwa uelewano jambo ambalo linachochea kuleta maendeleo kwa wakazi wa manispaa ya Iringa na kukuza uchumi kwa wananchi wake.