Mzee wa Mila wa Kabila la Wairaqw Mzee Amatli Buxu akitoa maelekezo ya kimila kuhusu namna kinywaji cha asili ya Kabila hilo aina ya Mangure kinavyo paswa kutayarishwa kabla ya kugaiwa kwa watu Mwenyekiti wa Jamii ya Wairaqw , Dkt Baltazary Awe akishiriki kikamilifu kwenye Tamasha hilo kwa kuburudika na kinywaji aina Magure kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho Bw Mawazo Ramadhani Jamvi akizungumza na Jamii ya Wairaqw waishio Dar Es Salaama na waliotoka Manyara kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
Mhe Balozi Dkt Wilbad Slaa akizungumza na Jamii ya Wairaqw waishio Dar Es Salaama na waliotoka Mkoa wa Manyara kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
Bw Reginald Malley kulia akielekezwa na mzee wa mila kutoka Manyara namna ya kucheza bao la asili ya kabila la Wairaqw kwenye Tamasha la kabila hilo lililofanyika Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam
WAIRAQ WATIKISA DAR ES SALAAM
Jaimii ya Wairaqw waishio Dar Es Salaam (UMBLUCHA) wamefanya tamasha kubwa Kijiji cha Makumbusho Dar Es Salaam kwa lengo la kuhakikisha jamii ya kabila hilo wanaoishi mijini hawaachi mila na desturi zao, kuwarithisha watoto hasa wanaozaliwa na kuishi mijini, pamoja na kuibua mawazo ya Utalii wa mazao ya Utamaduni.
Akizungumza na wanajumuhia ya kabila hilo Mgeni rasmi katika tamasha hilo Mhe Balozi Dkt Willibrod Slaa amewahasa watanzania hasa wazazi kuhakikisha wanaurithisha urithi wa utamaduni kwa kizazi kipya kwani kwa kupitia urithi huo muhimu watoto wataendela kukua katika maadali mema.
Dkt Slaa amempongeza Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye uhifadhi wa utamaduni wa matanzania hasa kwa serikali anayoingoza kuhakikisha imetenga hela kwa ajili ya kuboresha Kijiji cha Makumbusho kilichopo chini ya Makumbusho ya Taifa nchini.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa nchini Dkt Noel Lwoga, Kaimu Mkurugenzi wa Kijiji cha Makumbusho Bw Mawazo Ramadhani Jamvi amesema Taasisi hiyo imejiwekea utaratibu wa kushirikiana na Makabila mbalimbali katika kufanya matamasha ya kiutamaduni yenye lengo la uhifadhi na urithishaji wa urithi wa utamaduni.
Licha ya kuwapongeza Jumuia ya Wairaq waishio Dar es Salaam kwa kuamua kuratibu tamasha hilo, Bw Jamvi amewahakikishia kuwa Makumbusho ya Taifa itaendela kuwa karibu nao na hata kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya kabila hilo unafanyika kwenye Kijiji hicho ili kuutangaza na kuhifadhi urithi wa kabila hilo.
Dkt Leonia Hambati ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, amesema yeye amejisikia fahari kuendelea kudumisha utamaduni wake awapo mjini na anafanya hivyo kwa watoto wake bila kuangalia elimu yake wala mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayo chochoa kasi ya Utandawazi ambao unaharibu mitazamo ya vijana kuhusu utamaduni wao.
Akiongea kwa niaba ya Jamii ya Wairaqw (UMBLUCHA) waishio Dar es Salaam, Dkt Baltazary Awe amefafanua kuwa, jumuhia yao imeona umuhimu wa kufanya tamasha hilo ili kujikumbushia mambo yanayohusu Utamaduni wao, kuhakikisha watoto wao wanajifunza kutoka kwa wazee waishio vijijini, na kuowaonesha wengine utajiri uliopo kwenye utamaduni huo.
Tamasha hilo lililochukuwa siku mbili na kufurahiwa na wageni wa ndani na nje ya nchi, lilipambwa vyema na Ngoma za asili za kabiala hilo, vyakula vya asili, majigambo, masimulizi ya wazee nyakati ya husiku, Mapishi ya Pombo maarifu ya kabila hilo ijulikanoayo kama Magure, Michezo ya Jadi, dua kutoka kwa wazee wa mila walio ombea nchi, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya Tanzania pamoja na Muungano nk.