MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,akifungua kikao cha wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,akiwasisitiza jambo washiriki wa kikao cha wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akielezea mada mbalimbali zinazohusu kikao cha wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Bw. Nathalis Linuma,akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu kwa shule za Msingi na Sekondari wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Afisa Taaluma Mkoa wa Dodoma Bw.Abdallah Migila,akitoa taarifa ya ufaulu kwa Mkoa wa Dodoma ulivyoongezeka wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Dodoma Dk.Godfrey Mbabaye akizungumzia miradi ya maji inayotekelezwa katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Mhandisi wa Mipango,Usanifu na Ujenzi DUWASA Mhandisi Norbert Mwombeki,akiyoa taarifa ya utekeleza wa miradi pamoja na upatikanaji wa Maji katika Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma,akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya watu waliopata chanjo ya UVIKO-19 wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai,akichangia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Chemba Mh Mohammed Moni,akitoa maoni mbalimbali kwa wajumbe wa kikao wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Bw. Sosthenes Kibwengo,akichangia mada, wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili mbaga,akizungumza wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Emmanuel ,akichangia mada wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
Washiriki mbalimbali wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Wajumbe wa kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAKUU wa wilaya zote za Mkoa wa Dodoma wameagizwa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kabla ya Desemba 28,mwaka huu bila kuwepo na kisingizo chochote.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika jijini Dodoma.
Mtaka amesema kuwa ni ajabu kuona kiongozi aliyeteuliwa na Rais kushindwa kutekeleza jukumu hilo ndani ya wakati huku mikoa mingine wameweza.
“Lazima kama kiongozi wewe mwenyewe uwe na kiu ya kufanikisha jambo fulani haiwezakani leo eti kiongozi unasubiri kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa siku aliyopanga waziri Ummy ya Desemba 31.
“Hiyo ni siku ya waziri lakini na wewe unatakiwa kuwa na tarehe yako kama leo unaulizwa wewe utakamilisha lini utajibu Desemba 31 kweli hapana lazima viongozi tuwe na tamaduni zetu wenyewe lakini lazima tujifunze kwa wenzetu mbona Kigoma wenzetu wamemaliza na kukabidhi tayari”amesisitiza Mtaka
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Bw. Nathalis Linuma amesema kuwa mkoa umepokea Sh. 16,164,937,108 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu kwa shule za msingi na sekondari.
Naye Afisa Taaluma Mkoa wa Dodoma Bw.Abdallah Migila amesema kuwa jumla ya wanafunzi 40,355 wamefaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2022.
“Idadi hii ya wanafunzi ni ongezeko la wanafunzi 5,140 kulinganisha na idadi ya wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2020 ambapo wanafunzi 35,215 walifaulu”amesema