Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa Wabunge Sports Club, Mhe.Abbas Tarimba zilizotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) ikiwa ni kwa kuthamini mchango wa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki katika shughuli za uhifadhi wa misitu pamoja na utalii.
Mwakilishi wa Kamishna Uhifadhi wa TFS ,Neema Mawanja wamesema TFS inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Wabunge katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu hivyo zoezi la kuwakabidhi jezi leo ni ishara tosha kuwa mchango wao umekuwa wa maana sana katika kukuza na kuendeleza utalii wa kiikolojia
……………………………………………………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi kwa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki kama sehemu ya kuongeza chachu ya uhifadhi wa misitu na utalii nchini Tanzania.
Akikabidhi jezi hizo leo katika Uwanja wa Sheik Amri Abed uliopo jijini Arusha, Dkt.Ndumbaro amesema jezi hizo zimetolewa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambazo yeye alikabidhiwa kwa ajili ya kuwakabidhi Wabunge hao.
” Leo nimeweza kukabidhi vifaa hivi vya michezo kwa wabunge ili viwasaidie katika mazoezi na safari za kimichezo hivyo nakushukuru Mwenyekiti wa Bunge Sports Club kwa kukubali kupokea jezi hizi,”alisema Dkt.Ndumbaro
Dkt. Ndumbaro amesema TFS imejikuta ina kila sababu ya kukabidhi vifaa vya michezo hivyo kwa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki ikiwa ni kutambua mchango wa dhati unaotolewa na wabunge hao katika kulinda na kuhifadhi rasilimali misitu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani Tanzania
Dkt. Ndumbaro amesema jezi hizo zitasaidia kuongeza hali kwa wabunge Sports Club ili kuwawezesha kuweza vizuri zaidi kwenye michezo hivyo anashukuru viongozi mbalimbali kwa kuonyesha ushirikiano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wabunge Sports Club, Mhe. Abbas Tarimba amesema anamshukuru Waziri Ndumbaro pamoja na TFS kwa kuwasaidia kutoa jezi hizo ambazo zitakuwa chachu ya kuhamasisha jamii kuhifadhi wa misitu pamoja na kutembelea maeneo ya utalii hususani utalii wa kiikolojia
”TFS ni miongoni mwa Taasisi zinzofanya vizuri sana katika kulinda na kuhifadhi misitu, Misitu mingi tunayoiona ni kazi ngumu inayofanywa na Watumishi wa TFS kupitia Jezi hizi tutaendelea kuwa Mabalozi wa Uhifadhi wa misitu nchini” alisisitiz Mhe. Tarimba
Katika hatua nyingine, Mhe. Tarimba amesema vilevile Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanasijikia fahari kupata jezi hizo kutoka katika taasisi za kiserikali katika michuano hiyo ya michezo mbalimbali kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).
“Kama mnavyojua tangu michezo hiI ya Wabunge ianzishwe hatujawi kushinda kwa kishindo kama mwaka huu na hizi jezi ambazo tumepewa leo ni chachu ya kuendelea kuipenda Tanzania na mashindano mengine yajayo tutakuwa na vifaa vya kutosha na tutang’ara sana,” alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake MwaklisHI wa Kamishna Uhifadhi wa TFS,Neema Mawanja amesema wanatambua mchango unaotolewa na wabunge katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu.
Mawanja amesema Wabunge ndio watunga sera na sheria ambazo zinasaidia kulinda na kuhifadhi misitu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo hivyo kamishna wa uhifadhi ameona ni vyema kuutambua huu mchango wa wabunge.
“Kutokana na kutambua mchango wa wabunge wetu akaamua amkabidhi Waziri jezi kwa ajili ya wabunge wetu kwa Mbunge yetu ya Jumuiya ya Afrika mashariki,”amesema Mawanja