Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akivishwa skafu na skauti alipowasili Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma leo Desemba 18, kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa pili kushoto) akikagua mazingira ya chanzo cha maji kilichopo milima ya Matogoro Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo Desemba 18, 2021 wakati wa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu Wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa pili kushoto) akikagua mfumo wa majitaka alipokagua machinjio ya kisasa ya Manispaa ya Songea leo Desemba 18, 2021. Wengine pichani wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Steven Ndaki.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa pili kushoto) akikagua bwawa la majitaka alipofanya ziara ya kukagua machinjio ya kisasa ya Manispaa ya Songea leo Desemba 18, 2021. Wengine pichani wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Steven Ndaki.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua hifadhi ya misitu na chanzo cha maji katika milima ya Matogoro wilayani Songea mkoani Ruvuma leo Desemba 18, 2021 wakati wa ziara yake ya kikazi.
…………………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewataka wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji kwa kuepuka ukataji miti ovyo hasa maeneo ya milimani.
Dkt. Jafo ametoa wito huo alipotembelea na kukagua hifadhi ya misitu na chanzo cha maji katika milima ya Matogoro wilayani Songea mkoani Ruvuma leo Desemba 18, 2021 wakati wa ziara yake ya kikazi.
Katika ziara hiyo alionesha kuridhishwa na usimamizi mzuri wa misitu iliyopo katika eneo hilo ambalo maji yaje hutumika kuwahudumia wananchi wa Manispaa ya Songea kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SOUWASA).
“Ndugu zangu haya maji yanatiririka kwasababu ya utunzaji wa misitu hii na mimi naamini inawezekana katika maeneo mengine uharibifu wa mazingira umeshaanza na inawezekana uharibifu wa maji ungekuwa haujatokea ingewezekana tungekutana maji yanaoverflow (yanafurika).
“Hatuwezi kupata haya maji kama uharibifu wa mazingira ungekuwa mkubwa kwa mfano leo hii hawa watu wangeamua kufyeka misitu yote kwa ajili ya mkaa au kuni hiki chanzo maana yake kitakuwa ni ghost project (mradi hewa) yaani kutakuwa hakuna maji yoyote yanayotiririka maana yake kama Songea kuna upungufu wa lita za maji milioni sita kwa siku ambapo vyanzo vya maji ni hii milima ya hii ya Matogoro, hali ya Mji wa Songea itakuwa ni mbaya sana,” Waziri Jafo alitahadharisha.
Hivyo aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti kwa wingi hususana kwenye vyanzo vya maji na kuitunza ili kuepusha uhaba wa maji.
Pia waziri huyo alitolea mfano katika safu za milima ya Uluguru mkoani Morogoro ambayo vyanzo vyake vya maji vimeanza kukauka kutokana na uchomaji wa misitu kwa ajili ya mkaa na kuni hali inayosabanisha uhaba wa maji katika maeneo hayo.
Alitoa rai kwa viongozi wa mikoa, wilaya na Wakala Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha wanachukua hatua kali za kisheria kwa yeyote anayefanya shughuli inayohatarisha usalama wa vyanzo vya maji na mazingira kwa.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo alitembelea na kukagua mazingira katika machinjio ya kisasa iliyopo Manispaa ya Songea ambapo alionesha kuridhishwa na usimamizi wa mazingira.
Katika ziara hiyo alikagua mabwawa ya majitaka ambayo yatatumika kwa ajili ya kuhifadhi majitaka kutoka katika machinjio hiyo bila kutiririka ovyo katika maeneo ya makazi.
Licha ya kuupongeza uongozi wa halmashauri hiyo unaotekeleza mradi huo wa machinjio Waziri Jafo alitoa rai ya kuutunza na kuusimamia vyema ili pasitokee uharibu wowote.