Naibu Waziri Wazara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wahitimu wakati wa Mahafali ya Nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kisangara Naibu Waziri Wazara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Mwanaidi Ali Khamis akitoa cheti kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri wakati wa Mahafali ya Nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya KisangaraNaibu Waziri Wazara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Mwanaidi Ali Khamis akiwa katika maandamano ya Kitaaluma wakati wa Mahafali ya Nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kisangara, Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kisangara wakifurahia kuhitimu katika picha ya pamoja wakati wa Mhafali ya Nne ya Kampasi hiyo
Picha zote na Ofisi ya Uhusiano Taasisi ya Ustawi wa Jamii
*************************
Na Mwandishi Wetu Kisangara
Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kisangara iko mbioni kuanzisha kozi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtotokatika ngazi ya cheti na stashahada itakaotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
Jitihada hizi zinakuja mara baada ya hivi karibuni kuzinduliwa kwa Prorgamu ya Kitaifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya mwaka 2021/2022- 2025/2026.
Hayo yamsemwa na Naibu Waziri Wazara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Mwanaidi Ali Khamis katika Mahafali ya nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii – Kampasi ya Kisangara ambapo jumla ya wahitimu 524 wamehitimu.
Mh. Mwanaidi amesema suala hili litasaidia Taasisi kukua kitaaluma na kuongeza idadi ya wataalamu katika fani ya Ustawi wa Jamii. Na hii pia itasaidia Wizara kuendelea kutoa huduma bora kwa makundi maalum nchini kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii.
Ameongeza kuwa Wizara itaainisha maeneo ya ushirikiano kati yake na Taasisi na kupanga mikakati ya pamoja ya kuwatumia wahitimu katika utoaji wa huduma kwa jamii, tafiti na ushauri wa kitaalamu.
“Wizara kama mlezi wa Taasisi tutaendelea kuiangalia Taasisi hii kwa jicho la kipekee mno” alisema Naibu Waziri Mwanaidi.
Mh. Mwanaidi ameeleza kuwa Taasisi kupitia kampasi ya Kisangara inazalisha wataalamu wa fani ya Ustawi wa Jamii na fani ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kada ambayo ni muhimu sana katika utekelezaji wa mipango ya Wizara.
Ameongeza kuwa Wizara pia imeweka miongozo, kanuni na sheria mbalimbali katika kuhakikisha suala la malezi ya mtoto yanatolewa kitaalamu katika nyanja zote za kijamii kuanzia ngazi ya familia hadi kwenye makao na vituo vya kulelea watoto mchana.
“Napongeza mipango ya Taasisi kutaka kuanzisha programu ya shahada ya Ustawi wa Jamii katika mwaka wa masomo 2022/2023. Hakika hii itasaidia Taasisi kukua kitaaluma na kuongeza idadi ya wataalamu katika fani ya Ustawi wa Jamii.” Alisema Mh. Mwanaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jmaii Dkt. Joyce Nyoni amesema kuwa Serikali kupitia, Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka huu wa masomo wameletea wanafunzi katika ngazi ya cheti cha msingi katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara.
”Kwetu sisi hili linatuonyesha kuwa Taasisi yetu imeaminiwa kuwa ni sehemu na salama ya kuwasaidia vijana hawa kufikia malengo yao ya kitaaluma.” Alisea Dkt. Joyce.
Nao baadhi ya wahitimu wa mahafali ya Nne ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara wamesema watakwenda kutumia taaluma walioipata hasa katika Malezi, Mkauzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoa elimu sahihi kwa jamii katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora.