Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Mawaziri kutoka nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika wakati alipowasili katika Ukumbi wa Hoteli ya Lake Tanganyika Mkoani Kigoma kwajili ya kufungua mkutano wa tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza wakati wa ufunguzi mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Viongozi mbalimbali wakifatilia hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wanaoshiriki Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba 16,2021. ( kutoka kushoto kwa Makamu wa Rais ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande, Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira kutoka Zambia Mhe. Collins Nzovu, Waziri wa Mazingira , Kilimo na Mifugo kutoka Burundi Mhe. Deo-Guide RUREMA na Waziri wa Uvuvi na Mifugo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo Mhe. Adrien Bokele).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wanaoshiriki mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika mara baada ya kufungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya lake Tanganyika mkoani Kigoma. Desemba
………………………………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 16 desemba 2021 amefungua Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Nchi wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika unaofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Lake Tanganyika mkoani Kigoma. Mkutano huo unashirikisha Mawaziri wa Mazingira kutoka Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Zambia.
Akifungua Mkutano huo Makamu wa Rais ametoa wito kwa nchi wanachama wa usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika kushiriki kikamilifu katika kutoa michango yao ya ushiriki ikiwemo ada ya mwaka ya uanachama huo ili kuwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uhifadhi endelevu wa ziwa Tanganyika. Amesema Tanzania wakati wote ipo tayari kikamilifu katika kushirikiana na nchi wanachama katika kutekeleza mkataba wa usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika kwa maendeleo endelevu ya ziwa hilo.
Aidha Makamu wa Rais amesema ziwa Tanganyika limeendelea kuwa ziwa namba mbili duniani kwa kina pamoja na uwingi wa maji huku likihudumia zaidi ya watu milioni 10 wanaolizunguka ziwa hilo na kubarikiwa kuwa na viumbe visivyopatikana mahali popote duniani hivyo mawaziri hao wanapaswa kutafakari na kutoa njia zitakazowezesha ufuatiliaji wa taratibu zilizowekwa katika nchi wanachama kukabiliana na uchafuzi wa ziwa, uvuvi juu ya kiwango pamoja na mmomonyoko wa udongo.
Pia amewataka mawaziri kutoka nchi wanachama wanaoshiriki mkutano wa tisa wa usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika kutumia mkutano huo kama msingi wa kuongeza makubaliano na ushirikiano na kuwezesha mamlaka ya usimamizi ya ziwa Tanganyika kuongeza manufaa ya matumizi ya ziwa hilo kwa vizazi vya sasa na baadae.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande amesema kuanzishwa kwa ushirikiano huo kulilenga kubaini matishio na changamoto za uharibifu wa mazingira katika ziwa Tanganyika ambapo mpaka sasa faida mbalimbali zimepatikana zikiwemo kutekeleza kwa pamoja mpango wa maendeleo wa kanda wa ziwa Tanganyika, kuandaa mkakati wa ulinzi wa Bioanuai na usimamizi endelevu wa maliasili katika ziwa Tanganyika.
Naye mwenyekiti wa mkutano huo Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira kutoka Zambia Mhe. Collins Nzovu amesema ili kukabiliana na uharibifu wa ziwa Tanganyika nchi wanachama zinapaswa kuweka mkazo katika maendeleo ya kijani kwa kuweka sera kulinda mazingira wakati wa mipango ya maendeleo ya kiuchumi pamoja na kupunguza uzalishaji gesi joto.