Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akimkabidhi Nakala ya Mapango Kabambe wa mkoa wa Dar es Salaam 2016-2036 wakati wa hafla ya kukabidhi mpango huo mkoani Dar es salaam
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi Mapango Kabambe wa mkoa wa Dar es Salaam 2016-2036 tarehe 16 Desemba 2021. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akimkabidhi Nakala Laini za Mpango Kabambe wa mkoa wa Dar es Salaam 2016-2036 kwa ajili ya wakuu wote wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo kwa Mkuu wa Mkoa Amos Makala wakati wa hafla ya kukabidhi mpango huo
Picha ya sehemu ya jiji la Dar es Salaam ambayo miundombinu yake ya barabara imeboreshwa
…………………………………………………….
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amezitaka mamlaka za upangaji katika mkoa wa Dar es salaam kuandaa mpango maalum wa uendelezaji maeneo yote yenye miundombinu mikubwa ili uendane na thamani ya miundombinu husika.
Aidha, alizitaka mamlaka hizo za upangaji kuboresha mandhari ya maeneo yenye miundombinu mikubwa na kuwezesha shughuli za kibiashara na uwekezaji kwenye majengo.
Waziri Lukuvi alisema hayo tarehe 16 Desemba 2021 wakati wa uzinduzi mpamngo Kabambe wa mkoa wa Dar es Salaama 2016-2036 uliofanyika jjijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Lukuvi katika serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo uwekezaji kwenye viwanda na ujenzi wa miundombinu unatiliwa mkazo na kupewa msukumo jitihada za kuboresha miundombinu ukiwemo utekelezaji miradi ya barabara za mabasi yaendayo kwa kasi (BRT) na upanuzi wa barabara thamani ya miundombinu iliyopo haiakisi aina ya uendelezaji unofanyika kwenye uso wa huduma hizo muhimu.
‘’Katika Serikali ya awamu ya sita ambapo ujenzi wa miundombinu unatiliwa mkazo na kupewa msukumo kama vile upanuzi wa barabara ya morogoro na ile ya Ally Hassan Mwinyi kutoka mjini hadi Mwenge lakini thamani ya miundombinu haiakisi aina ya uendelezwaji unaofanyika uso wa huduma hizo’’ alisema Lukuvi.
Akielezea Mpango Kabambe aliouzindua , Lukuvi alisema mpango huo ambao utekelezaji wake utafanyika kwa kipindi cha miaka 20 kuanzia 2016 hadi 2036 unalenga kutoa fursa za kuboresha huduma na kuondoa chanagamoto zilizobainika huko nyuma.
Alisema, Mpango Kabambe wa mkoa wa Dar es Salaam unalenga kuendeleza jiji kwa mfumo shindanie na ndelevu kwa manufaa ya watu. Pia mpango huo unapendekeza kuweka masharti mapya katika kuendeleza upya maeneo katika jiji kwa kuzingatia kuongeza uwiano wa ujenzi wenye lengo la kuongeza matumizi ya ardhi kwa ujenzi wa majengo ya magorofa.
Aidha, Mpango huo Kabamabe unazingatia pia kuongeza ujazo wa kiwanja ambapo ujenzi katika jiji la Dar es Slaam utakuwa ukianzia ghorofa nne na kuendelea.
Kupitia Mpango huo Kabambe, Waziri Lukuvi alisema vitaanzishwa vitovu vipya vya huduma ili kupunguza msongamano eneo la kati la jiji na kubainisha kuwa vitovu hivyo ni Mwenge, Ubungo, Kurasini, Mbezi, Tangibovu, Tazara, Kibada, Kongowe, Pugu Kijiungeni, Mpiji magowe, Bunju, Ukonga, Mbagala, Kigamboni Ferry na maeneo mengine na kusisitiza kuwsa vitovu hivyo vyote vitakuwa masharti kulingana na sifa za maeneo.
Aidha, alisema Mpango utaweka mfumo wa usafiri mbadala ya kitovu kimoja cha huduma katika jiji ambayo inatengeneza mfumo wa barabara za miale zinazoelekea eneo la kati ya jiji na kusisitiza kuwa mpango huo unapendekeza kuwepo ujenzi wa barabara za mzunguko na ujenzi wab barabara za mabasi yaendayo kasi ili kupunguza foleni na mahitaji ya usafiri.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala alisema, Mpango Kabambe uliozinduliwa kwenye mkoa wake ni kwa ajili ya kuendeleza jiji kwa mfumo shindani na kusisitiza kuwa mabadiliko yanayoenda kufanyika katika mkoa wake hayataenda kuvunja nyumba za wananchi bali kutoa fursa ya hadhi ya eneo husika.
Mpango Kabambe wa kwanza kuandaliwa nchini uliandaliwa kwa jiji la Dar es Salaam mwaka 1949 ikiwa ni manispaa ya Dar es Salaam na ule wa awamu ya pili ulifanyika mwaka 1968 na awamu ya tatu mwaka 1979 na kutokana na ukuaji wa kasi wa jiji katika kipindi ambacho hakukuwa na mpango changamoto mpya zilijitokeza zikiwemo za kijamii, kiuchumi na kimazingira.