Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati akifungua mkutano wa Wadau wa kujadili hali ya Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa nchini Tanzania uliofanyika leo Desemba 15,2021 Jijini Dodoma .
Wadau wa Siasa nchini wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani),wakati akifungua mkutano wa Wadau wa kujadili hali ya Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa nchini Tanzania uliofanyika leo Desemba 15,2021 Jijini Dodoma .
……………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza msajili wa vyama vya siasa nchini na Jeshi la Polisi kukaa pamoja na wadau wa Demokrasia nchini kujadiliana namna bora itakayo tumiwa na vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara bila kuvunja sheria za nchi.
Rais Samia,ametoa maagizo hayo leo Desemba 15,20201 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili hali ya Demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Rais Samia amemtaka msajili wa vyama vya siasa kutumia mkutano huo kukaa pamoja na jeshi la polisi na wadau hao ili kujadilina namna sahihi ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara bila ufunjifuu wa sheria.
“Makae mjifunge wenyewe na mapendekezo hayo myalete kwetu sisi tutapitia na tukiona yanafaa tutaruhusu mikutano ya hadhra lakini tukiona bado kunamapungufu hatuta ruhusu”amesema Rais Samia
Pia amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuutumia mfumo wa vyama vingi kama sehemu ya kuwapa wananchi mdala wa nini watafanya kusaidia maendeleo ya nchi.
“Siasa siyo matusi, siyo kuchafuana siyo kuchonganisha wananchi na serikali yao,lakini pia siasa siyo ugomvi siasa inatumika kama sehemu ya kuleta maendeleo na fikra tofauti katika kusaidia kujenga taifa ”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, amesema hotuba ya Rais Samia imefungua ukurasa mpya kwa wanasiasa wa Tanzania.
”Hotuba ya Rais imetoa mwanga wa kupatikana kwa mardhinao ya kisasa ambayo vyama va siasa vilikuwa vinayatarajia kwa muda mrefu”amesema Prof.Lipumba