Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma leo Desemba 15,2021.
Seleman Yondo, Kaimu Mrugenzi wa Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI,Seleman Yondo,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma leo Desemba 15,2021.
Mkuu wa kitengo cha Chakula, Maji na Usafi wa Mazingira Wizara ya Afya,Anyitike Mwakitalima,akitoa mada wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma leo Desemba 15,2021.
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya Mazingira na Usafi, Wizara ya Afya Dk. Khalid Massa,akielezea hali ya watu kuwa na vyoo unavyoongezeka nchini wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma leo Desemba 15,2021.
Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma leo Desemba 15,2021.
……………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe,amewataka maafisa afya nchini kusimamia sheria ya usafi wa mazingira na kuwachukulia hatua kali watu wote wasio kuwa na vyoo.
Pia amesema, Suala la Utunzaji wa Mazingira ndio msingi wa Afya Bora kwa wananchi na ndio inasaidia jamii kuondokana na magonjwa mbalimbali ikiwepo kipindupindu ambacho chanzo chake kikuu ni ulaji wa kinyesi/uchafu.
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 15,2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi unaondelea jijini Dodoma.
Dkt.Magembe amesema kama maafisa hao watazingatia usafi wa mazingira ni wazi kuwa magonjwa ya kuambukiza yatakwisha katika jamii kama ambavyo kipindipindi kilivyo dhibitiwa mkoani Dar es Saalam.
“Asilimia 70 ya kaya zenye choo nchini bado ni kiasi kidogo sana hatupaswi kujisifu inabidi kutoka sasa kuongeza nguvu ili asilimia hii ifikie 100 hakikisheni kila kaya inakuwa na choo chake siyo kushea vyoo vya kushea ni kwenye taasisi kama vile shule, hospitali lakini siyo makazi”amesema Dkt.Magembe
Amesema asilimia kubwa ya magonjwa yanasababishwa na uchafu wa mazingira kama jitihada zitawekwa kwenye sekta hiyo hali itabadilika.
Amesema kuwa alipokuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliwahi kumng’ang’ania mtu aliyetupa uchafu kupitia dirisha la gari na alipo kaidi nilisimama kwenye msingi wa sheria hadi akapokea adhabu inayo mstahiki, hivyo lazima mjue dhamana mliyopewa ni kubwa ni vema mkaitendea haki
Hata hivyo amewataka maafisa hao kuendelea kuwekeza katika elimu kwa jamii juu ya usafi wa mazingira na kuachana na adhabu za kuwabambikizia watu.
“Wekezeni katika elimu acheni kubambikiza faini watu wa mabucha na hoteli hiyo itakuwa biashara toeni elimu ya kutosha kwa jamii ili watu wabadilike lakini watakao kuwa wabishi sheria itumike mara moja”amesisitiza
Awali akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Masuala ya mazingira nchini, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya Mazingira na Usafi, Wizara ya Afya Dk. Khalid Massa,amesema kwa sasa hali ya watu kuwa na vyoo bora nchini imeongezeka kutoka asilimia 42 ya mwaka 2017 na kufikia asilimia asilimia 70 kwa mwaka 2021.
Dkt. Massa amesema, katika kipindi hicho kutokana na mikakati waliojiwekea wameweza kupunguza kaya zisizo kuwa na vyoo kutoka asilimia 9.6 hadi kufikia asilimia 1.3 kwa mwaka 2021, vilevile wameongeza vyombo vya kunawia mikono kwenye kaya kutoka asilimia 5.6 ya mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 41.7 kwa mwaka 2021, lakini pia wameendelea kuchukua hatua za kulinda mipaka kwakuwa ajiri na kuwapeleka vijana wapatao 70 kwa ajili ya masuala ya Afya Mazingira mipakani.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Afya Mazingira na Usafi unafanyika jijini Dodoma, ukiwa na lengo lakujitathmini juu ya utendaji kazi wao na kuweka mikakati kwa ajili ya Mwaka ujao, Mkutano unaongozwa Kaulimbiu isemayo Uimarishaji wa huduma za Afya Mazingira na usafi katika mapambano ya Uviko -19