Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Manfredo Fanti, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (tatu-kushoto) akikata utepe kuashiria kwa uzinduzi wa mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akiangalia vifaa mbalimbali mara baada ya kuzindua mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
Washiriki mbalimbali wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi ,uliofanyika jijini Dodoma.
………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna, DODOMA
SERIKALI imejipanga ifikapo mwaka 2025 kuzalisha Megawati 1100 za umeme jua na upepo ambapo kwa mwaka huu zitazalishwa Megawati 150.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizindua mradi wa kusaidia matumizi endelevu ya nishati ya Jadidifu kwa ajili ya kupikia na Mradi unalenga zaidi kwenye kilimo kwa kutumia umeme jua katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliowakutanisha serikali na wadau wa sekta binafsi.
Byabato amesema vyanzo ambavyo ni vizuri vinavyolinda mazingira na havigharimu maisha ya binadamu ni upepo na jua.
“Tukipata umeme kwa njia ya upepo na jua ni jambo ambalo haliishi ndio maana linaitwa renewable, mpaka sasa tuna kiwango kidogo sana cha umeme unaotokana na hizo nishati mbadala,”amesema.
Amebainisha kuwa umeme mwingi unatoka kwenye gesi asilimia 60, kwenye maji ni asilimia 30 na kwamba litakapokamilika bwawa la Mwalimu Nyerere litaongeza kiwango cha uzalishaji umeme kwa kutumia maji.
“Tumejipanga kuhakikisha kwamba mwaka huu tunapata angalau Megawati 150 kwa kutumia jua na upepo na tayari tumeanza kusaini mikataba kati ya TANESCO na Wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali madogo ambao wataweka mitambo yao ili kuzalisha umeme wa kutosha,”amesema.
Kadhalika, amesema wamepanga ifikapo mwaka 2025 katika vyanzo vikubwa vya umeme kuwe na Megawati 1100 zinazotokana na jua na upepo.
“Tumefanya upembuzi yakinifu kwenye baadhi ya maeneo na tumegundua tunaweza kupata umeme wa jua kwenye eneo fulani, tunatangaza tender ili mtu yeyote anaweza kuja na kuweka vifaa vyake na kuzalisha umeme, sisi TANESCO na yeye tunakubaliana bei kununua umeme halafu sisi tuingize kwenye gridi yetu,”amesema.
Awali Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Manfredo Fanti,amesema kuwa Mradi ambao umezinduliwa ni sehemu ya mashirikiano baina ya Umoja wa Ulaya na Tanzania kwa upande wa sekta ya nishati.
”Mradi huo ni muhimu kwasababu utatoa mchango mkubwa katika kupunguza matumizi ya mkaa hasa katika maeneo ya mjini na vijijini”amesema
Aidha ameeleza kuwa mradi huo hautasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira tu lakini pia utasaidia kuimarisha afya za watu kwakuwa hewa itokanayo na moshi wa matumizi ya mkaa na kuni unamadhara kwa afya ya mtumiaji.
Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nishati Jadidifu Tanzania, Prosper Magali, ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wa sekta binafsi katika kutimiza dhamira yao.
“Ni mambo ambayo yametupa faraja kuona kwamba tayari nishati jadidifu imetengewa mchango wake katika upatikanaji wa umeme, sisi kama sekta binafsi tupo tayari na tulitamani kiwango hicho kilichosemwa kiongezeke zaidi kwasababu tunao wadau wa ndani na nje ambao wapo tayari kuwekeza kwenye eneo hili,”amesema.
Ameongeza “Tunatamani serikali ingeongeza kiwango hicho kwa kuwa Megawati 1000 ni ndogo kwa wadau wa ndani na nje, hata hivyo tunashukuru serikali kwa kutambua mchango wetu na kututengea kiwango hicho, lakini tungetamani kiongezeke zaidi.”
Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi Mkuu, Uwekezaji na Fedha kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji na Maendeleo, Emmanuel Muro, amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo watawajengea uelewa wananchi kwa kuwapa semina ya nishati hizo ili wajue matumizi yake na mahala pa kuipata.
“Tutatoa elimu na kufanya kazi na watu mbalimbali ikiwamo wafanyabiashara, tutatoa ruzuku ambapo kutakuwa na vigezo ambavyo kila mmoja atapaswa kufikia, lengo ni kuwawezesha watanzania kufanya nishati ya kupikia kama bidhaa inayouzika na yenye mfumo na kuhitaji jitahada mbalimbali za wadau wa maendeleo, serikali,”amesema.
Amebainisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa miaka mitatu kwa gharama ya Euro milioni 17 ili kusaidia utunzaji wa mazingira.