Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Makao Mkauu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faidha Suleiman akikabidhi misaada ya vyakula kwa watoto wenye ulemavu wa Shule ya Msingi Mitindo Wilayani Misungwi ikiwa ni sehemu ya ziara ya Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania bara na Zanzibar mkoani Mwanza.Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Emmanuel Mziba na Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza Mrakibu wa Polisi (SP) Joyce Kotecha
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Makao Mkauu ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faidha Suleiman akitoa elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwa Wasafiri, Madereva,Makondakta na Wafanyabiashara katika Stendi ya Mabasi ya Buzurugwa mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya ziara ya Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania bara na Zanzibar mkoani Mwanza.Watendaji hao pia Wametoa elimu katika Stendi ya Nyegezi, Mialoni na Vituo mbalimbali vya bodaboda
Watendaji mbalimbali wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Tanzania bara na Zanzibar wakiendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya ziara ya Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoani Mwanza.Watendaji hao pia Wametoa elimu katika Stendi ya Nyegezi, Mialoni, Masokoni na Vituo mbalimbali vya bodaboda (Picha na A/INSP Frank Lukwaro wa Jeshi la Polisi)