Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akikabidhi Tuzo ya kipengele cha Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia (Technology and computer science) zilizoandaliwa na Young Scientists Tanzania (YST Awards ceremony 2021) kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro, Innocent Mamsery (kushoto) na Sylvester Mulungu (kulia) ambao walibuni mradi wa mfumo wa kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kielimu (Academic Progress Analysis System). Vodacom Tanzania Foundation ni taasisi inayosaidia vumbuzi mbalimbali zitakazoipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali.
Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akizungumza kwenye hafla ya Tuzo za Young Scientists Tanzania (YST Awards ceremony 2021) Vodacom Tanzania Foundation ni mdhamini wa tuzo hizo pia ni taasisi inayosaidia vumbuzi mbalimbali zitakazoipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali.
Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro, Sylvester Mulungu namna anavyoandaa miradi mbalimbali hususani miradi ya maendeleo ya wanafunzi kielimu, ikiwa sehemu ya maonesho ya Young Scientists Tanzania 2021