Washiriki katika maonyesho ya kwanza ya kazi za ubunifu wa Tehama wakifuatilia maonyesho hayo yaliofanyika Ukumbi wa skuli ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
Mkurugenzi Tehama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Omar S. Ali akiangalia baadhi ya kazi za ubunifu wa tehama zilizofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA katika maonyoesho ya kwanza ya siku ya UBUNIFU WA TEHAMA yaliyofanyika Ukumbi wa Skuli ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Prof. Mohammed Makame Haji akizungumza na kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia katika maonyesho ya kwanza ya kazi za ubunifu wa tehama huko Ukumbi wa Skuli ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
Mkurugenzi Tehama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Omar S. Ali akifungua maenyoshe ya kwanza ya ubunifu wa tehama kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, huko Ukumbi wa skuli ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
Mkurugenzi Tehama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Omar S. Ali (wakwanza kulia) akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa kuskani namba za bidhaa ili kuweza kutambua ubora wa bidhaa hiyo,maelezo hayo yakitolewa na Mbunifu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa SUZA Mohammed mshimba seif wakati wa maonyesho ya kazi za UBUNIFU WA TEHAMA yaliyofanyika Skuli ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR.