Naibu Kamishna Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Hazina (Hazina Saccos) uliofanyika leo Desemba 11,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Hazina (Hazina Saccos) Bw. Aliko Mwaiteleke akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama hicho uliofanyika leo Desemba 11,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanachama wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Hazina wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema, (Hayumo pichani) wakati wa Mkutano uliofanyika leo Desemba 11,2021 jijini Dodoma.
Naibu Kamishna Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Hazina (Hazina Saccos) uliofanyika leo Desemba 11,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Hazina (Hazina Saccos) kuweka malengo ya kuweka akiba kwa siku, mwezi, mwaka hadi ya kustaafu.
Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dionisia Mjema kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Mwigulu Nchemba,wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nane wa Mwaka wa Hazina Saccos Ltd uliofanyika leo Desemba 11,2021 jijini Dodoma.
Dk.Nchemba amewataka kuweka akiba ili kutekeleza malengo waliyoweka ya muda tofauti. Pia watambue kwamba uimara wa chama unatokana na kiwango kikubwa cha akiba wanazoweka wanachama wake.
”Utamaduni wa kuweka akiba unaanzia nyumbani, hivyo wanatakiwa kudumisha utamaduni huo wa kuweka akiba ambako kunatokana na kujinyima leo kwa ajili ya kesho kwa ajili ya kutekeleza malengo yaliyowekwa na mtu binafsi, taifa na dunia kwa ujumla”amesema Dk.MwiguluAidha Dkt.Nchemba amekipongeza Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, (Hazina Sacoss) kwa kutekeleza agizo la Serikali la kushusha riba za mikopo kwa wanachama wake kutoka asilimia 12 hadi asilimia 11 kwa mwaka.“Sacoss ni nyenzo muhimu ya kupambana na umasikini, kujenga uchumi wa kaya kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla hivyo ni muhimu kuwa na sacoss imara na endelevu ambayo inatatua changamoto za wanachama”, amesema Dkt. Nchemba.Hata hivyo Dk.Nchemba amewataka wanachama hao kuongeza michango kwenye chama ya kila mwezi ili kuongeza uwigo wa kupata mikopo zaidi.Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Hazina Sacoss Bw. Aliko Mwaiteleke,amesema kuwa wamejipanga kuwa chama chenye mlengo wa kutoa huduma bora kulingana na mahitaji na changamoto zinazowakabili wanachama wao.‘’Chama chetu kinatarajia kuongeza kiwango cha kukopa hasa mikopo ya dharura kwa wanachama wetu kutoka shilingi milioni mbili (2,000,000/-) mpaka shilingi milioni tano (5,000,000/-)’’ amesema Bw. Mwaitekele