Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. RoseMary Mwaipopo akizungumza katika Kongamano la kitaaluma kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo. Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George akielezea umuhimu wa Teknolojia katika Kongamano la kitaaluma kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Extended Impression Paul Patrick akielezea namna alivyotumia wazo la kibunifu alikuwa nalo kuanzisha Kampuni katika Kongamano la kitaaluma la Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. RoseMary Mwaipopo akipokea tuzo kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George katika Kongamano la kitaaluma kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. RoseMary Mwaipopo akitoa tuzo kwa Melita Kanafunzi mmoja wa mwanafunzi waliofanya vizuri katika eneo la taaluma wakati wa Kongamano la kitaaluma kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo. Baadhi ya wanafunzi na wahitimu kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakifuatilia Kongamano la kitaaluma kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
********************
Na Mwandishi Maalum Tengeru Arusha
Inaelezwa kuwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ni moja ya Taasisi muhimu katika kuleta mabadiliko katika kuleta maendeleo nchini ikiwa ni sehemu inayozalisha wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanaotumika kutatua changamoto katika jamii.
Hayo yamebainika leo mkoani Arusha katika Kongamano la kitaaluma lililofanyika katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii kuelekea Mahafali ya 11 ya Taasisi hiyo.
Akizungumza katika Kongamano hilo Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. RoseMary Mwaipopo amesema Taasisi hiyo amesema wahitimu wa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kutumia ujuzi wao katika kusaidia kutatua changamoto na kuchagiza katika fursa mbalimbali.
Dkt. Rosemary amewataka wahitimu wa Taasisi hiyo kujitathimini ni nini wanaweza kufanya katika kuisaida jamii inayowazunguka hasa katika kuhakikisha wanatafuta namana sahihi ya kutumia fursa zilizopo kutatua changamoto za ajira.
“Naomba mjitathimini mkalete mabadiliko katika jamii mkatumie elimu mliyoipata hapa mlete matokeo chanja kwaajili ya amendeleo ya jamii ” alisema Dkt. Rosemary
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George ameeleza kuwa wahitimu kutoka katika Taasisi hiyo wanatakiwa kutumia teknolojia iliyopo kama fursa ya kutafuta namna ya kupata ajira au kujiajiri katika sekta mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Extended Impression Paul Patrick amesema kuwa wahitimu wa Vyuo wanatakiwa kuwa na udhubutu wa kufanya mabadiliko katika jamii kwa kuajiriwa na kujiajiri ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii.