Naibu katibu Mkuu UTUMISHI,Dkt.Michael Francis, akiongoza kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mbunge Jimbo la Mpanda Mjini,Mhe.Sebastiani Simon Kapufi,akichangia mada katika kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mratibu,Kitengo cha Taaluma za Rushwa,Dr Alfred Sebahene, wa chuo kikuu cha st. John akichangia hoja katika kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mweneykiti ya Kamati ya Maadili ya Chuo Kikuu cha Dodoma,Dr Ombeni Msunya,akichangia hoja kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CPCT Dodoma,Mch.John Maliga,kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Abdallah Chaurembo, akizungumza katika kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Neema Mwakalyelye ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa tuungane unaotekelezwa kati ya TAKUKURU kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kutoka nchini Ujerumani kilichofanyika Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja
…………………………………………………………….
Na.Erick Mungele,Dodoma
WADAU wa mradi wa mapambano dhidi ya rushwa ujulikanao “Tuungane kutetea Haki awamu ya pili unaotekelezwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU] kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung[KAS] kutoka nchini Ujerumani wamependekeza Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini iangaliwe upya kwa lengo la kusaidia kuwabana Zaidi viongozi ikiwemo kujiuzulu nafasi zao kwani kutaifishwa mali zao pekee haitoshi.
Aidha wadau hao ni pamoja na Viongozi wa TAKUKURU Mkoa,na Wilaya viongozi wa dini sambamba na waratibu vitengo vya taaluma za rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kikao hicho,Mwenyekiti wa kikao hicho Dkt.Francis Michael ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kutaifishwa kwa mali pekee haitoshi hivyo kuna haja kubwa ya kuangalia upya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
“Utaratibu huu wa kuwataifisha mali zao halafu wanaendelea na shughuli zao kiukweli haijakaa sawa na haitoi hofu kwani mtu anajua nikitaifishwa mali zangu ajira yangu inabaki kuwa pale pale TAKUKURU inabidi ikae itazame upya sheria hii” amesema Michael
Kwa upande wake Omben Msuya Mwenyekiti kamati ya Maadili ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) amesema TAKUKURU kupitia watoa elimu waendelee kusambaza elimu ya rushwa katika vyuo kwa wanafunzi ili waelewe haki zao na kujua namna ya kutopokea au kutoa rushwa.
“Tunaona kiukweli jitihada ambazo Takukuru wanazifanya lakini elimu hii isambazwe kwenye vyuo ili wanafunzi wetu waendelee kuelewa rushwa ni nini”amesema Dk.Msuya.
Kisusu Mvumbo ni Kadhi wa Mkoa wa Dodoma ameshauri TAKUKURU katika kuendeelea na mapambano hayo dhidi ya rushwa watoa elimu watembelee nyumba za ibada na kuomba kutumia japo dakika 15 kuelimisha waumini kuhusu rushwa.
Mvumbo amesema pamoja na kutoa elimu hiyo kanisani na misikitini lakini pia watumie vyombo vya habari zikiwemo radio na televisheni kuielimisha jamii kujua haki zao ili kusiwepo na mianya ya utoaji wa rushwa.
Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Neema Mwakalyelye amesema lengo la mradi wa tuungane ni kuwashirikisha wadau ngazi za vijiji na mitaa hadi Taifa namna ya mapambano dhidi ya rushwa huku meneja mradi wa KAS Tanzania Damas Nderumaki akisema matarajio ya sasa ni kufikia mikoa 24 .
“Tumejipanga kusambaza elimu hii mashuleni,misikitini,makanisani, watendaji wa mitaa kuwashirikisha katika vikao vya halmashauri na pia mtaala mashuleni tunaendelea kujipanga elimu hii ianzie katika shule ya msingi ili watoto wawe na uelewa kuhusu rushwa”amesema Neema
Kwa upande wao baadhi ya wadau wa mradi wa Tuungane akiwemo Naibu Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania Abdallah Sakasa,mbunge wa Mbagala,Abdallah Chaurembo pamoja Afisa Uchunguzi TAKUKURU Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Ilandike Julius wamesema kikao hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa .
Wamesema wao kama wadau wa mapambano dhidi ya rushwa kupitia mapendekezo yaliyotolewa katika kikao kazi hicho yakiwemo ya kutoa elimu katika jamii ikiwemo misikitini,makanisani, shuleni na mitaala kuangaliwa upya wanaamini ya kwamba endapo yatatekelezwa kwa ufanisi kwa kiasi kikubwa watakuwa wamejitahidi katika mapambano dhidi ya rushwa .