…………………………………………………
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amewakumbusha Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na UVIKO -19 ili kukabiliana na Wimbi la Nne la mlipuko wa janga hilo unaoendelea kuleta athari ulimwenguni
Ametoa wito huo leo kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru na miaka 59 ya Jamhuri ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga yamefanyika leo ili kutoa nafasi kwa Wananchi kushiriki maadhimisho ya kitaifa kesho Disemnba 09.
Amesema kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kupitia wataalamu wa afya.
“Tunapoendelea na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kuutumikia mkoa wetu na Taifa kwa ujumla, tuchukue tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu ya Covid 19 sote tunafahamu kuwa ugonjwa huu hupo katika mataifa mbalimbali tuchukue tahadhari na kuzingatia miungozo yote inayotolewa na wataalam wa afya”
Mkuu wa Mkoa huyo Sophia Mjema ameekeza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu uhuru mwaka 1961 katika sekta mbalimbali ambapo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kujenga uchumi imara katika Mkoa wa shinyanga na Taifa kwa ujumla
“Katika sekta zote Elimu, Afya, Kilimo, Barabara na sekta zingine zimeongezeka kwa kadri serikali inavyoongeza fedha na kuweza kuhudumia mikoa tuendelee kuunga mkono serikali yetu ili tuweze kuondokana na ule uchumi wa chini na tufike katika uchumi wa kati”
Leo Disemba 09,Watanzania wataadhimisha Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo kitaifa kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salam huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema “MIAKA 60 YA UHURU TANZANIA IMARA NA KAZI IENDELEE”